…………………………………………………………………….
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Baraza la madiwani halmashauri ya jiji la Arusha limemchagua Diwani wa Kata ya Kaloleni Maxmillian Iraghe kuwa Mstahiki Meya wa jiji hilo baada ya kuwabwaga wenzake Isaya Doita na Prosper Msofe.
Akiongea wakati akimtangaza mshindi huyo Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.John Pima ambaye ndio msimamizi wa uchaguzi huo akitangaza matokeo alisema Maxmilliani Iraghe amepata kura 29 akifuatiwa Prosper Msofe aliyepata kura 9 huku Isaya Doita akiambulia kura 2.
Alisema kwa mamlaka ya kisheria anamtangaza rasmi Maxmillian kuwa Mstahiki Meya wa halmashauri hiyo ya jiji la Arusha kuongoza baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano.
Mara baada ya kutangazwa mshindi Mstahiki Meya aliwashukuru madiwani kwa kuonyesha imani kubwa kwake na kuahidi ushirikiano na kufanyakazi kwa kasi na weledi wa hali ya juu.
Alisema kuwa baraza hilo chini yake litakuwa ni baraza la kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo katika kipindi chote atakachokuwa madarakani.
Aliwaomba wananchi kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake naye atajitahidi kuendeleza ushirikiano na kuchapakazi usiku na mchana kuwaletea maendeleo wananchi wa jiji la Arusha.
“Watendaji na madiwani huu sasa ni muda wa kuchapakazi kuhakikisha ilani ya CCM inatekelezwa kwa kiwango cha juu kila moja wetu aliahidi kuwatumikia wananchi kwa nguvu zote tukaonyeshe hilo sasa”
Kwa Upande Mwengine Mkurugenzi wa Jiji la Arusha alimtangaza naibu Meya wa Jiji hilo kuwa ni Veronica hosea Diwani wa vitu maalumu kutoka kata ya Moshono
Mara baada ya kutangazwa aliwashukuru madiwani kwa kuonyesha imani juu yake na kuahidi kuchapakazi katika kumsaidia Mstahiki Meya kwenye majukumu ya kuongoza baraza la madiwani ndani ya jiji la Arusha.
Alisema kuwa misingi yake ya uongozi ni kuchapakazi na ushirikiano kwamadiwani na watendaji ndani ya halmashauri hivyo kuhakikisha yale malipo kwenye ilani ya chama cha mapinduzi yanatekelezwa kwa vitendo.
“Niwasihi sana tupeni ushirikiano nasi tutachapakazi kutekeleza shughuli za kuwaletea maendeleo wananchi wetu”