Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, wakimsikiliza Wakili Mkuu wa Serikali Ndg. Gabriel Malata wakati akizungumza nao kabla ya kumkabidhi nyaraka mbalimbali Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende mapema leo. Kabla ya kuwa Wakili Mkuu wa Serikali Ndg. Malata alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.
Wakili Mkuu wa Serikali Ndg. Gabriel Malata (ambaye alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali) akimkabidhi ofisi kinyaraka Dkt Bonipace Luhende katika hafla fupi iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akitoa neno la shukrani mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi hiyo kinyaraka mapema leo katika hafla iliyofanyika ndani ya ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.