*******************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ameridhishwa na hatua ya Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Ubungo ambapo amewaelekeza Suma JKT kuhakikisha Ujenzi wa Hospital hiyo unakamilika na kukabidhiwa kabla ya January 08 ili Wananchi waweze kuitumia.
RC Kunenge ametoa maelekezo hayo wakati alipotembelea Ujenzi huo na kujionea majengo Sita kati ya Saba yakiwa Katika hatua ya upauaji ambao kwa mujibu wa mkandarasi Ujenzi umefikia 60%.
Aida RC Kunenge amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kuridhia kutoa fedha za Ujenzi huo ili kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi wa Ubungo ambao kwa muda mrefu walikuwa wakisafiri Hadi Sinza kufuata huduma.
Pamoja na hayo RC Kunenge amewapongeza JKT kwa kazi nzuri wanayoifanya pamoja na uongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa usimamizi madhubuti wa Mradi huo.
Kwa upande wake Luteni Kanali Edward Antony ambae ni Mkurugenzi wa Viwanda SUMA JKT amemuhakikishia RC Kunenge kuwa Ujenzi huo utakamilika na kukabidhiwa ndani ya wakati.