Wabunge Wateule wa Viti Maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo – wakisubiri kula kiapo kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo.
SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Halima Mdee kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo
SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Esther Matiko kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo.
SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Esther Bulaya kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo.
SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Cecilia Pareso kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo.
Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Halima Mdee akiongea jambo kwa niaba ya Wabunge wengine wa CHADEMA walioapishwa hii leo kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Viti Maalum CHADEMA walioapisha hii leo kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi na Bunge)
…………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Hatimaye Wabunge19 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamesalimu amri na kuamua kuwaapishwa rasmi na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai.
Baada ya kuwaapisha Spika Ndugai ameahidi kuwalinda, kuwatetea na kuwapa ushirikiano,ili kukamilisha jukumu la kikatiba katika kuwatumikia wananchi.
Spika Ndugai amesema kuwa Novemba 20 mwaka huu alipokea barua kutoka tume ya taifa ya uchaguzi ikimjulisha uteuzi wa wabunge hao 19 wa viti maalum.
Wabunge hao walioapishwa ni pamoja na Halima Mdee, Grace Tendega, Ester Matiko, Cecilia pareso, Ester Bulaya, Agnester Kaizer, Nusra Hanje, Jesca kishoa, Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo
Wengine ni Asia Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majela,Stella Fihaya, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchester Lwamlaza.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wabunge wengine, Mbunge wa Viti maalum Halima Mdee amesema kuwa watanzania wanapaswa kuelewa kuwa nafasi hiyo haikutolewa kama hisani bali ni sehemu ndogo ya ushindi mkubwa ambao chama chao kimeupata.
Mdee amewahakikishia wanachama wa CHADEMA kuwa wabunge hao watafanya kazi kwa uaminifu kipindi chote watakachokuwa Bungeni kwa kuweka mbele maslahi ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuilinda katiba ya chama chao.
Mbunge wa viti maalumu Ester Matiku amesema kuwa nadhani wote tunajua taratibu za viti maalumu za kuweza kufika kwa Mbunge wa kuteuliwa,kuna utaratibu ambao unaendelea ndani ya chama kupitia na baadae chama kinabariki na majina yanaenda kwenye tume ya taifa ya uchaguzi.
“Binafsi nilitaarifiwa na mamlaka husika kuwa nimeteuliwa ndio maana nimefika hapa kuja kuapa”amesema Matiku.
Matiku amesema kuwa watatumia nguvu zote,akili zote na kwa hekima zote kuhakikisha kuwa wanawakilisha chama vizuri ndani na nje ya bunge lakini pia kuwatetea watanzania amabao wengi wao wanaimani na chama hicho
Hata hivyo wabunge hao waviti maalum wameapishwa baada ya kupita siku 15 tangu kuanza kwa bunge la 12 Mkutano wa kwanza wa mwaka 2020 uzinduliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli