Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Biharamulo Robert Alphonce Malulu aliyesimama akiongea kwenye kikao cha madiwani wa CCM kwaajili ya kumchagua mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Madiwani wateue wa CCM wakimsikiliza mkurugenzi wa uchaguzi aliyesimama Adia Mamu Rashid ambaye ni katibu wa CCM wilaya Biharamulo kwenye kikao cha kumchagua mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Mhe.Eng. Ezra John Chiwelesa aliyesimama akiongea na madiwani wateule wa halmashauri ya wila Biharamulo kwenye kikao cha kumchagua mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Madiwani ateule wa CCM wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wao wa chama mara baada ya kumchagua mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi Mhe. Eng. Ezra John Chiwelesa kushoto akimpongeza mwenyekiti wa halmashauri aliyechaguliwa Mhe. Rushahu Leo Mathew kulia mara baada ya zoezi la uchaguzi kuisha.
(Picha zote na Allawi Kaboyo)
*************************************
Na Allawi Kaboyo – Biharamulo.
Madiwani wateule wa halmashauri ya wilaya Biharamuro kupitia Chama Cha Mapinduzi wamefanya uchaguzi wa kumteua mwenyekiti atakayeliongoza baraza la madiwani hao pamoja na makamo mwenyekiti ambapo wameelekezwa kuhakikisha halmashauri hiyo inapanda kiuchumi.
Akiongea katika kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Mwenyekiti wa CCM wilaya Biharamulo Robert Alphonce Malulu ameeleza kuwa chama hicho hakiidhishwi na ukusanywaji wa mapo ya halmashauri hiyo hali iliyompelekea kuwataka madiwani kuwa wakali ili kuhakikisha mapato ya halmashauri yanaongezeka.
Malulu amesema kuwa halmashauri hiyo inazo raslimali nyingi hivyo haina sababu ya kuwa miongoni mwa halmashauri za mwisho katika ukusanyaji wa mapato kwa miaka mingi mfurulizo huku miradi mbalimbali ikishindwa kutekelezwa kwa kukosa fedha.
“Mimi niseme tu Biharamulo ni tajiri sana, sema halmashauri hii ilikosa usimamizi mathubuti na kutupelekea kuwa halmashauri ya pili kutoka mwisho katika ukusanyaji wa mapato, jambo hili sisi kama chama hatuliungi mkono na wala hatutataka kuliona tena, niwaombe madiwani shikamaneni katika kuhakikisha mapato yanapatikana ukizingatia hapa nyote mnatokana na CCM.” Amesema Malulu.
Kwaupande wake mbunge wa jimbo hilo Mhe. Mhandis Ezra John Chiwelesa ambaye pia alikuwa mjumbe kwenye kikao hicho amesema kuwa kwasasa wananchi wa Biharamulo wanataka kuona mabadiriko ambayo wameahidiwa kwenye kampeni na hatimaye kuamua kuwachagua.
Amesema kuwa Madiwani ni nguzo kubwa katika ukusanyaji wa mato na kupanga bajeti ambayo hutekeleza miradi mbalimbali ya maenedeleo kwa wananchi hivyo katika kipindi hiki wanatakiwa kuwa wakali na kuona uchungu katika fedha za serikali kwa kuhakikisha zinatumika inavyotakiwa.
Ezra ameongeza kuwa yeye kama mbunge atatoa ushirikiano mkubwa kwa madiwani wote kwa kuhakikisha changamoto zote alizoziona kwenye maeneo hayo kipindi cha kampeni zinapatiwa ufumbuzi, na kuongeza kuwa madiwani wasikubali kutumiwa na mtu ambaye anamasahi binafsi na kusababisha kuwa na matabaka.
“Kama mnakumbuka waheshimiwa madiwani Mhe.Rais Magufuli wakati wa kuapishwa alisema uchaguzi umekwisha tena kwa msisitizo akarudia mara tatu, name niseme uchaguzi umekwisha na huu ndo ulikuwa uchaguzi wa mwisho ndani ya chama hivyo tuondoe makundi na tuwe kitu kimoja kwaajili ya wanabiharamulo.” Amesem Ezra.
Rushahu Leo Mathew ni mwenyekiti aliyechaguliwa na madiwani kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambapo amewashukuru madiwani kwa kumuamini na kusema kuwa atatumia uzoefu alionao katika halmashauri hiyo kuhakikisha anaitoa halmashauri ilipo kimapato na kuisogeza mbele huku akiahidi kutetea maslahi ya madiwani kwa kuhakikisha wanalipwa kwa wakati.
Katika uchaguzi huo nafasi ya mwenyekiti wa Halmashauri wagombea walikuwa wawili huku wapiga kura wakiwa 24 ambapo Mhe. Rushahu amechaguliwa kwa kura 13, mwenzake ambaye ni Mwalimu Antius Bruno akipata kura 10 na kura moja ikiwa imeheribika.
Kwaupande wa makamo mwenyekiti aliyechaguliwa ni Mihayo Rutambi aliyepata kura 14 dhidi ya mpinzani wake Mhe. Erick aliyepata kura 10 na hakuna kura iliyoharibika.