baadhi ya wakulima wa kilimo cha umwagiliaji katika kijiji cha Nakahuga
wakifuatilia mkutano na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Mkulima katika skimu ya kilimo cha uwagiliaji ya Nakahuga iliyopo
Peramiho wilayani Songea Bw. Albert Mtani akiuliza swali wakati wa
mkutano na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Na Mwandishiwetu – Peramiho
Wakulima
katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Nakahuga iliyopo Peramiho
wilayani Songea mkoani Ruvuma wameipokea sheria ya Taifa ya kilimo cha
umwagiliaji na kuonesha utayari wa kuchangia katika mfuko wa maendeleo
yakilimo cha umwagiliaji kwa kukiri kuilewa sheria hiyo mara baada ya
mafunzo waliyopata toka kwa wataalam kutoka Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji.
Akizungumza wakati wa mkutano wa majumuisho
uliofanyika katika kijiji cha Nakahuga,mmoja wa wakulima hao Bw. Albert
Mtani alisema kuwa kilimo cha umwagiliaji kwao ni mkombozi kwani ni
kilimo cha uhakika.
“Binafsi ninaishukuru serikali kwa kuleta
mradi huu nani naamini inania njema ya kuendelea kuboresha miondombinu
katika skimu hii na kwa kuwa tunapata faida nyingi zitokanazo na
shughuli zetu zakilimo, hivyo sio ni tatizo kwenye uchangiaji katika
mfuko kwani ninaamini kuwa mifereji itakapo haribika kwa namna yoyote
ile serikali itaitengeneza kupitia mfuko huo, na tutaendelea na
shughuli zetu za kilimo bila wasiwasi.” Alisema.
Sambambana hilo
kwa nyakati tofauti katika ushiriki wa mkutano huo, baadhiya wakulima
walisikika wakisema kuwa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji sasa imekaa
vizuri kwani kabla yakuwepo kwa sheria hiyo ushirikishwaji wa wakulima
kuhusu shughuli za umwagiliaji ulikuwa ni mdogo na kulikuwa na usimamizi
mbovu wa miundombinu yaumwagiliaji
Waliongeza kwa kusema kuwa
sheria ya Taifa ya umwagiliaji pia itaweza kusaidia kutatua migogoro
midogo midogo iliyopo katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji.