………………………………………………………………………………….
Na.Mwandishi Wetu
Timu ya Yanga imeshindwa kuishusha kileleni Azam FC baada ya kulazimshwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC mechi wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kipindi cha kwanza timu zote zilienda mapumziko zikiwa zimefunga Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa kiungo wao mshambuliaji Carlos Carinhos dakika ya 13 na dakika ya 16 Stephen Sey akaisawazishia Namungo.
Kipindi cha Pili timu zote mbili zilifanya mabadiliko kwa kushambuliana kwa kasi mnamo dakika ya 90 Namungo walipata Penalti baada ya Mwamnyeto kumchezea rafu ndani ya kumi na 8 hata hivyo Blaise Bigirimana alikosa.
Shujaa wa Yanga wa Ni Mlinda Mlango Metacha Mnata ambaye amepangua Penalti katika dakika ya 90 yaani za lala salama.
Kwa matokeo hayo Yanga wanabaki katika nafasi ya pili wakiwa na Pointi 25 sawa na Azam FC wenye pointi 25 ila wakiwa wako juu ya tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga.