********************************************
DODOMA
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Komred Kheri D James leo ametembelea na kukagua eneo litakalo jengwa Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, katika Shughuli hiyo ameambatana Na Viongozi wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Dodoma pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanao wakilisha Kundi la Vijana.
Ujenzi wa Ofisi hiyo ya Makao Makuu una tarajia kuanza hivi karibuni na kuwekwa jiwe la msingi mwanzoni mwa mwezi Januari Mwaka 2021.
Aidha Komred Kheri amezungumza Na Wenyeviti na Makatibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya zote za CCM Jijini Dodoma wakiongozwa Na Mwenyekiti wa Mkoa huo Ndg Billy Chidabwa Katika kikao kilichofanyia Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma.
Katika Kikao hicho komred Kheri amewapongeza Viongozi hao kwa kazi nzuri waliyofanya katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.