Mshambuliaji Mzambia wa Azam FC, Obrey Chirwa akiwa chini ya ulinzi wa beki Ismail Gambo na kipa Juma Kaseja wa KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. KMC imeshinda 1-0 bao pekee la Reliant Lusajo dakika ya 57.