Meneja wa NMB tawi la Mpanda Alex Massawe (anayeonekana katikati) akitoa somo kwa washiriki wa mkutano huo
Mmoja wa wakulima bwana Protus Ringo akiuliza swali katika mkutano huo wa kuwahamasisha wakulima kuchukua mikopo ya pembejeo.
****************************************
Na Zillipa Joseph
Wakulima wa mkoa wa Katavi wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na taasisi za kifedha katika kuchukua mikopo ya pembejeo ili kuinua kuwawezesha kufanya kilimo biashara na kukuza pato lao
Rai hiyo imetolewa na meneja wa benki ya NMB tawi la Mpanda mkoani katavi Alex Massawe wakaati akifungua mkutano maalum na wakulima na wafanyabishara wa mkoa huo
Massawe amesema benki hiyo imekuwa ikikutana na wakulima wa maeneo tofauti kwa lengo la kutoa elimu ya kilimo biashara ambayo itamsaidia mkulima kuleta tija katika kilimo
“Hii ni mara ya kwanza kwa NMB kufanya mkutano maalum na wakulima kwa hiyo ni vyama mkaitumia fursa hii ili kupata mafanikio ya haraka” alisema Massawe
Akizungumzia mikopo hiyo ya pembejeo Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kilimo bwana Wogofya Mfalamagoa amesema benki inatoa mikopo ya pembejeo za aina tofauti kwa wakulima ambapo rejesho lake ni mara moja tu kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitatu
“Mathalani tunakupa trekta unafanyia kazi rejesho lake ni moja tu kwa mwaka, sio mnakwenda mabenki mengine mmnakutana na rejesho la kila mwezi! Sisi tunaangalia nguvu ya uwekezaji iliyofanyika” alisema
Aidha Mwakilishi kutoka NMB foundation Rogers Shipela amethibitisha kuwa taasisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima
“Taasisi ya NMB foundation imeundwa kwa lengo la kutoa mafunzo ya ujasiriamali ambapo mkulima ataweza kuuza mazao yake kwa bei itakayomnufaisha pamoja na hilo tunatoa elimu ya masoko ambayo inatolewa ili mkulima aweze kuuza mazao yake kwa ufanisi “alisema