Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akizungumza na wauza matunda katika soko la Bunju B leo wakati alipofika kwa ajili ya kusikiliza kero zao.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akizungumza na wakina mama wajasiriamali wa Nyanya katika Soko la Bunju B.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akiwa ameongozana na Viongozi wa Soko la Bunju B alipokuwa mefika kwa ajili ya mkutano na wajasiriamali wa Soko hilo.
Wajasiriamali wa Soko la Bunju B wakiwa kwenye mkutano na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Ndug. Kiduma Mageni akizungumza na wajasiriamali wa soko la Bunji B katika mkutano na Mkuu wa Wilaya Mhe. Daniel Chongolo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo wa kwanza kulia akijadiiana na jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ndug. Kiduma Mageni pamoja na Mkuu wa Idara ya fedha Ndug. Maximilan Tabonwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akizungumza na wajasiriamali wadogo wadogo katika Soko la Bunju B.
***************************************
Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo kwakushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, wameahidi kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ikiwa ni katika utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. John Magufuli yakutaka kundi hilo lipewe kipaumbele katika kutimiza shughuli zao.
Akizungumza na wajasiriamali hao wasoko la Bunju B leo, Mhe. Chongolo amesema kuwa Serikali iliyopo madarakani iko mstari wa mbele kuhakikisha inaboresha mazingira ya wafanyabiashara na wajasirimali wadogowadogo ili waweze kutekeleza majukumu yao bila changamoto yeyote.
Jumatatu Oktoba 17,saa tatu asubuhi Mgombea Urais, wa Chama Chamapinduzi CCM Dk. John oseph Pombe Magufuli alisimama hapa, kweli sio kweli, na alizungumza masuala kadhaa ikiwemo la Wamachinga kweli sio kweli, na aliahidi atasimamia masilahi ya wamachinga katika Wilaya hii, kweli sio kweli, sasa nasisitiza kwamba tunayafanyia utekelezaji” amesisitiza Mhe. Chongolo.
Ameongeza kuwa Mkuu wa Wilaya kama msimamizi mkuu wa shughuli za Serikali zihusuzo ulinzi na usalama wa raia wake ameahidi kushughulikia changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ikiwa ni pamoja na kulinda ulinzi na usalama wa mali pamoja na biashara zao.
“ Kiongozi Mkuu wa Serikali ndani ya Wilaya ya Kinondoni ni Mkuu wa Wilaya, sasa mbona mnaniambia habari ya kuhama kuhama, nani kasema kwamba atawahamisha hapa, hatuwezi kuwahamisha, lakini pia mmesema mko tayari kutafutiwa eneo la karibu,hilo jambo litafanyika kwa haraka” amesema Mhe. Chongolo.
Awali akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya huyo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bunju B, Athuman Njama amesema kuwa aneo ambalo wajasiriamali hao wanafanyashughuli zao kwa sasa ni rafiki kwa sababu linafikika tofauti na eneo ambalo walitakiwa kwenda.
Katika hatua nyigine, Mhe. Chongolo amewataka kuzingatia suala la usafi katika eneo ambalo wanafanya shuguli zao ili kuweka mazingira safi kwa watu ambao wanakuja kununua bidhaa katika eneo hilo.