*******************************
NJOMBE
Mtu mmoja anaedaiwa kujihusisha na masuala ya unyang’anyi na ujambazi anaefahamika kwa jina la Izack Kawogo ameuwawa na vikosi vya Polisi mjini Njombe baada ya kumjeruhi kaka yake anaefahamika kwa jina la Andreas Kawogo(61) kwa kumpiga risasi mbili begani kwa kutumia siraha aina ya SMG Uzgun.
Kamanda Issa amesema vikosi vya ulinzi na usalama vimemshambulia kwa risasi mtuhumiwa huyo ambaye tayari ni marehemu baada ya kumpiga risasi kaka yake kwa madai ya kwamba ameuza mali zake na kushindwa kumtoa gerezani wakati akitumikia kifungo.
Aidha Kamanda huyo amesema wakati uchunguzi unafanyika ili kumnasa mtuhumiwa ndugu walikuwa wazito kutoa ushirikiano licha ya kujua maovu yake jambo ambalo limesababisha kuchelewa kumdhibiti na kisha kutoa rai kwa wananchi na watu wenye tabia za wizi na ujambazi.
Kuhusu hatua zinazochukuliwa kwa siraha iliyopatikana baada ya kuibiwa gerezani Issa amesema wanakwenda kufanya utaratibu wa kuirudisha katika gereza ilipoibiwa