Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi,Emanuel Kayuni, akifungua kikao cha Baraza Dogo la wafanyakazi Jeshi la Zimamoto na Ukoaji leo jijini Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji John Masunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza Dogo la wafanyakazi wa jeshi hilo,akitoa taarifa wakati wa kikao cha Baraza Dogo la Wafanyakazi Jeshi la Zimamoto na Ukoaji iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu wa Baraza Dogo la Wafanyakazi ,Felix Mushi,akitoa neno la shukrani mara baada ya kufunguliwa kwa kikao cha Baraza Dogo la Wafanyakazi Jeshi la Zimamoto na Ukoaji lililofanyika leo jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi,Emanuel Kayuni (hayupo pichani) wakati akifungua kikao cha Baraza Dogo la wafanyakazi Jeshi la Zimamoto na Ukoaji leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi,Emanuel Kayuni akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha Baraza Dogo la wafanyakazi Jeshi la Zimamoto na Ukoaji kilichofanyika leo jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi,Emanuel Kayuni,amewataka wajumbe wa Baraza dogo la wafanyakazi wa jeshi la Zimamoto na Ukoaji kuondoka na ujumbe wenye majibu badala ya malalamiko ili kwenda kujenga katika sehemu zao za kazi.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza Dogo la wafanyakazi Jeshi la Zimamoto na Ukoaji,amesema kuwa kikao hiki ni muhimu katika kujadili matatizo yaliyopo ili kuyapatia majibu.
Bw.Kayuni amewataka wawakilishi kutoka mikoa tofauti kuwa watumie ipasavyo kikao hiki cha baraza kudai maslahi ya wafanyakazi wenzao ambao hawakuweza kufika,kwa sababu baraza ni sehemu sahihi ya kupanga mikakati ya kuboresha utendaji kazi.
Aidha amewaasa wajumbe wa baraza hilo kuwa makini kusikiliza agenda ambazo zitajadiliwa ndani ya kikao pamoja na kuchangia mada ili wakifika katika vituo vyao vya kazi ili waweze kuwaeleza wenzao kile walichojadili.
“Baraza la wafanyakazi ni muhimu katika sehemu ya kazi,hivyo wajumbe wawakilishi mnapaswa kubeba ujumbe wenye majibu ya kutatua changamoto mlizonazo badala ya kuondoka na ujumbe wa malalamiko unaokwenda kubomoa,”amesema Kayuni.
Awali Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji John Masunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza Dogo la wafanyakazi wa jeshi hilo,amesema kuwa vipaumbele vyao katika bajeti iliopita na ijayo ya 2021 ni upatikanaji wa vitendea kazi katika jeshi hilo ili kurahisisha utendaji kazi wa kila siku.
Kamishna Jenerali Masunga ,amesema kuwa watajadili bajeti iliopo na ijayo ya 2021 ili kuona namna ya kuifanyia kazi ili kuboresha utendaji kazi.
Aidha Kamishna Jenerali Masunga maesema kuwa Jeshi hilo linatoa huduma nyingi za uokoaji na si za moto pekee hivyo wananchi wanapaswa kutoa taarifa kwa wakati pindi wanapoona janga limetokeo.
”Sisi tayari tumejiwekea mikakati jinsi ya kukabiliana na majanga ya moto na mengine,tumeanzisha vituo 38 katika wilaya mbalimbali ambavyo vinasaidia katika utendaji kazi wetu”amesema Kamishna Jenerali Masunga
Amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni pamoja na kwenda na kasi ya ukuaji wa miji hivyo nao wanaendelea na ufunguaji wa vituo hivyo ili kuwarahisishia katika utendaji kazi.
“Naomba niwatoe hofu wananchi kuwa magari ya zimamoto hayana maji,yanakuwa nayo isipokuwa huisha na kwenda kuleta mengine,”amesisitiza Kamishna Jenerali Masunga.