Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.Leonard Subi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya matumizi ya choo Duniani ambayo huadhimishwa Novemba 19 ya kila mwaka leo jijini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.Leonard Subi, akizungumza kuhusu siku ya matumizi ya choo Duniani ambayo huadhimishwa Novemba 19 ya kila mwaka leo jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imewataka watendaji kuanzia ngazi za mashina kuhamasisha ujenzi wa vyoo na kuhakikisha kila mwananchi anatumia choo bora ili kujikinga na magonjwa mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.Leonard Subi ,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya matumizi ya choo Duniani ambayo huadhimishwa Novemba 19 ya kila mwaka lengo la siku hiyo ni kuona namna ambavyo wananchi wanaweza kutumia vyoo bora
Aidha Dkt.Subi ameitaja mikoa ambayo ipo chini kwa ujenzi na matumizi ya
vyoo bora kuwa ni pamoja na Kigoma,Lindi,Dodoma na baadhi ya mikoa ya
Kanda ya Ziwa ambapo kwa baadhi ya mikoa vinara kwa vyoo bora ni
pamoja na Dar es Salaam ,Iringa na Njombe
Dkt.Subi amesema kuwa lengo la siku hii ni kuimbusha jamii kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za afya ikiwa ni hatua muhimu ya kujikinga na maradhi yanayoenezwa kwa njia ya uchafu.
.
“Wiki ya Usafi wa Mazingira mojawapo ya mikakati mahususi ambayo inatumika kuibua na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa usafi katika ustawi wa jamii hasa katika Nyanja za Afya,elimu,maji na uchumi lakini pia siku hii ina lengo la kuikumbusha jamii kutumia vyoo bora ili kujikinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza”amesema Dkt.Subi
Dkt.Subi amesisitiza kuwa umuhimu wa ujenzi wa vyoo bora kwa jamii na maeneo yote yenye mikusanyiko pamoja na kuweka mazingira katika hali ya usafi wakati wote.
Hata hivyo amesema kuwa matumizi ya vyoo bora ni afya muhimu katika kujikinga na kudhibiti maradhi ya kuambukiza huku asilimia 40 ya magonjwa yanayosababishwa na uchafu yanaweza kuepukwa.
Aidha Dkt.Subi ameitaka jamii kuendelea kunawa mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara badala ya kufikiri zoezi lakunawa mikono liliishia kwenye maambukizi ya virus vya corona.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Zingatia usafi wa jinsia kwa usafi wa mazingira endelevu