Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Kiswahili (BAKITA), Bi. Consolata Mushi (kushoto) akifafanua jambo kwa Balozi wa Poland nchini Tanzania Mheshimiwa Krzysztof Buzalski (kulia) wakati wa hafla fupi ya kumtunuku cheti balozi huyo kwa kufuzu kujifunza lugha ya Kiswahili kwa wageni mapema hii leo katika Ofisi za BAKITA jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya BAKITA, Dkt. Method Samwel.
Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Kiswahili (BAKITA), Dkt. Method Samwel (kulia) akifurahia jambo na watumishi wa BAKITA( hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumtunuku cheti Balozi wa Poland nchini Tanzania Mheshimiwa Krzysztof Buzalski (hayupo pichani) kwa kufuzu kujifunza lugha ya Kiswahili kwa wageni mapema hii leo katika Ofisi za BAKITA jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa BAKITA, Bi. Consolata Mushi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Kiswahili (BAKITA), Dkt. Method Samwel (katikati) akimkabidhi cheti cha utambuzi wa ujuzi wa Kiswahili Balozi wa Poland nchini Tanzania Mheshimiwa Krzysztof Buzalski mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa BAKITA, Bi. Consolata Mushi.
Balozi wa Poland nchini Tanzania Mheshimiwa Krzysztof Buzalski (kulia) akitoa neno la shukrani mara baada ya kutunukiwa cheti cha utambuzi wa ujuzi wa Kiswahili kwa wageni mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Method Samwel na kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa BAKITA, Bi. Consolata Mushi.
Balozi wa Poland nchini Tanzania Mheshimiwa Krzysztof Buzalski (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Baraza la Taifa la Kiswahili (BAKITA) mara baada ya kutunukiwa cheti cha utambuzi wa ujuzi wa Kiswahili kwa wageni mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Kiswahili (BAKITA), Dkt. Method Samwel (kushoto) akimkabidhi cheti cha utambuzi wa ujuzi wa Kiswahili Balozi wa Poland nchini Tanzania Mheshimiwa Krzysztof Buzalski mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Eliphace Marwa
WHUSM – Dar es Salaam