KATIBU Mkuu wa Wizara
ya Mifugo na Uvuvi (Anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi) Dkt Rashid Tamatamah kulia akikagua ujenzi wa ofisi hiyo
KATIBU Mkuu wa Wizara
ya Mifugo na Uvuvi (Anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi) Dkt Rashid Tamatamah asema
uvuvi harama kwa kutumia mabomu nchini umepungua kwa asilimia 100 huku kwa
upande wa maziwa wakifanikiwa kudhibiti kwa asilimia 80.
Hatua hiyo imesaidia
kuongeza uzalishaji wa samaki ambao wanazalishwa hapa nchini kutoka miaka ya
nyuma mpaka sasa kutokana na udhibiti wa uvuvi haramu ambao umefanywa na
serikali.
Dkt Rashid aliyasema
hayo mjini Pangani wakati wa ziara yake ya siku moja ya kwenda kuangalia ujenzi
wa ofisi za BMU Kata ya Kipumbwi huku akionyeshwa kuridhishwa na kazi ya ujenzi
wake
Ujenzi unatekelezwa
na Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya ufadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia
mradi unaoitwa Swiofish na unafanya mambo mengi huo lakini moja vitu ambavyo
vimeazimiwa kutekelezwa vitu vya mwisho katika mradi huo wa miaka sita ambao
utaisha mwakani.
Alisema katika vitu
vya kutekelezwa ni kujenga majengo ya oifisi za BMU Tano kwenye ukanda wa Pwani
walitaka kila mahali wajenge lakini fedha zilizopo zilikuwa hazitoshi hivyo
wakachagua maeneo matano tu ambayo ni Lindi, Bagamoyo, Saadani, Kipumbwi na
Zingibar
Alisema wakati serikali
ya awamu wa tano katika kipindi chake ca kwanza ilipokuwa inanza kazi hali ya
uvuvi nchini ilikuwa mbaya sana kutokana na kukithiri kwa uvuvi haramu.
Alielez baada ya
serikali kuingia mwaka 2017 ikaamuliwa kwamba kama wataendelea hali hiyo
ingeendelea rasilimali za uvuvi zingetoweka na kama unavyojua uvuvi ni moja ya
sekta inayoajiri watu wengi wenye kipato cha chini kwa hiyo maisha ya watu yangebadilika.
“Hivyo serikali ikamua kuchukua hatua za makusudia
kuanzisha operesheni za uvuvi haramu kwenye maziwa waliita operesheni sangara
na kwenye ukanda wa pwani kulikuwa na operesheni Jodari ambazo ziliwasaidia
walikuwa wanawashirikisha BMU”Alisema Katibu Mkuu huyo.
“Lakini pia na watu waliokuwa wanaitakia mema
nchi yetu na taasisi za ulinzi na usalama hivyo baada ya mwaka mmoja matokeo
yalikuwa mazuri sana kwenye ukanda wa pwani ikiwemo maeneo ya Kigombe na Tanga
kwani uvuvi wa mabomu ulikuwa umekithiri kule Dar mabomu yalikuwa yakipigwa
mpaka pale karibu na Ikulu”Alisema
Alisema operesheni
hizo kwa upande wa pwani kuna meli za nje walikuwa wanapewa leseni za kuvua na
ilikuwa ya mashati kwamba wavua samaki wa aina fulani lakini wakawa wanavua
samaki ambao ni nje ya leseni.
“Kuna meli iliyokuwa
inatoka Vetnam ilikamatwa ikiwa na mapenzi ya papa ilishikiliwa Serikali
ikafungua kesi ikaendeshwa tukashinda ikapigwa faini ya Bilioni 1 au waende
jela hiyo wameenda jela”Alisema
Akizungumzia upande
wa Maziwa kwenye ziwa Victoria alisema wamefanikiwa kutokomeza uvuvi haramu kwa
zadi ya asilimia 80 lakini bado hawajamaliza kabisa huko na kubwa zaidi ilikuwa
ni matumizi ya nyavu haramu.
Alisema kutokana na
kudhibiti uvuvi haramu mafanikio yake yamekuwa makubwa sana samaki wameongezeka
kwa sababu mara ya kwanza wameweza kuvuka.
Alisema kwa sababu
miaka ya nyumba kote Tanzania haijawahi kuwa na samaki ambao wanazalishwa Tani
400,000 ambazo zinazalishwa kwa mwaka ambazo zilikuwa zinazalishwa zilikuwa ni
chini yake baada ya operesheni hizo kwa mwaka 2018/2019 kwa mara ya wamefika
tano 448,000 huku mwaka uliopita walipata tani 497,000.
Katibu huyo alisema
kwa upande wa ziwa Tanganyika samaki aina ya Sangara viwanda vingi vya minofu inayopelekwa
nje ni vya Sangara hivyo kuna viwanda huko ambavyo vilifungwa kutokana na uwepo
wa uvuvi haramu.
Alisema lakini pia
zamani nchini walikuwa na viwanda vya Tanzania 12 hadi 13 lakini kutokana na
uvuvi haramu nyingi vilikufa na kubaki 8 na vingi vilikufa kutokana na kukosa
malighafi .
Aidha alisema kwani
kulikuwa hakuna samaki na kupelekea viwanda ambavyo vilikuwa na uwezo wa
kuchakata tani 40 kwa siku vilikuwa vinachangakata tani 3 mpaka 5 kwa siku kwa hiyo
wafanyakazi ajira zilipotea.
“ Baada ya kufanikiwa
kukomesha uvuvi harama samaki wanapatikana wameongezeka na sio tatizo viwanda
vinazalisha muda wote na sasa kuna viwanda vinne ambavyo wanajengwa”Alisema
Hata hivyo alisema
katika kipindi cha awamu ya tano wanaendelea kutoa elimu na wavuvi hawamu wengi
wamebadilika na hiyo imewapa nguvu serikali ya awamu ya tano kipindi cha pili wajikite
kwenye ujenzi wa viwanda vya kuchakata samaki na kiuchumi kuwawezesha watu
wawezeke kwenye maeneo yote kuvua ambapo Rais Dkt John Magufuli amesema
atanunua meli nane ambapo nne zitakuwa Zanzibar na nyengine zitakuwa huko
Tanzania.