*******************************
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inampongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mbunge wa Ruangwa) kwa kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tume inamtambua Mhe. Majaliwa kama mdau na mshiriki mkubwa wa Tume katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na jamii inayoheshimu uhifadhi na ulinzi wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
Tume inamtakia Mh. Majaliwa kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yake katika kipindi cha miaka mitano ijayo.