Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli Masanja akionyesha vitu mbalimbali na badhi ya wazee na watemi kabla ya kusimikwa kuwa Mtemi wa Wasukuma na kuitwa jina la Masanaj au mkusanya watu.
Mtemi wa Kndi, wilayani Busega, Chifu Seni Wenceslaus akimvisha vazi la utemi Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli na kupewa na jina la Masanja jana hafla iliyofanyika kwenye Makumbusho ya Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Bujora jana.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli au Masanja , jana akipokea mkuki kutoka kwa Mtemi wa Lanadi Chifu Seni Wenceslaus (wa pili kushoto) na kutawazwa mtemi wa kabila laa Wasukuma.
Pokea usinga huu ikiwa ni ishara ya utawala bora ndivyo Chifu Seni wa Kanadi anavyomweleza Mkuu wa Wilaya ya Magu wakti wa kumsimika kuwa mtemi wa Wasukuma jana.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli aku Masanja akiwa amekalia kiti cha enzi utemi wa Wasukuma baada ya kusimikwa jana na Chifu Seni Wenceslau wa Kanadi ambaye pia ni Katibu wa Watemi, hafl iliyofanyika kwenye Makumbusho ya Utmaduni wa Kabila la Wasukuma Bujora.Picha zote na Baltazar Mashaka
……………………………………………………………………………
NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
Mtemi akimsimika Mkuu huyo wa Wilaya alisema wazee hao hawajakurupa kumpa wadhifa huo bali wamezingatia utendaji wake ukiambatana na mema aliyofanya kwa muda mfupi wilayani humo ikiwemo kuwakusanya na kuwaunganisha watu wa kada na rika mbalimbali .
“Amefanya na kutenda kwa wema,anafanya kazi nzuri na unaweza kuwa wa mfano kwenye nchi hii, utendaji wako huo wa kuwakusanya watu na kuwashauri hivyo nakuvisha vazi hili jesui ikiwa ni ishara ya mawingu yanayowezesha mvua kunyesha kwa niaba na manufaa ya jamii unayoiongoza,” alisema Chifu Seni.
Alifafanua kuwa usinga aliokabidhiwa ni ishara ya utawala ili awatawale na na kuwaongoza watu kwa hekima na busara akizingatia uongozi na utawala ulio bora kwani serikali inakuwepo badala ya Mungu.
Katibu huyo wa Watemi aliongeza kiti cha mtemi ni ishara ya kupewa madaraka kama alivyoteuliwa Mungu,yawe madaraka ya jadi au ya kiserikali.
Akizungumza baada ya kusimikwa Kalli alimuomba Mwenyezi Mungu amwongezee fikra na mawazo awaongoze kuwatumikia wananchi bila kujali makabila yao, rangi wala itikadi za dini na siasa.
Aliwashukuru wazee wa Kisesa na Bujora kwa kutambua mchango wake katika kuwatumikia na kuahidi kutobweteka bali atazingatia na utawala na uongozi ulio bora kuhakikisha anatatua kero na changamoto za wananchi wa Magu katika kufikia maendeleo yao na wilaya kwa ujumla.