Mwenyekiti wa Ulinzi Sekta Binafsi Tanzania, Felix Kagisa akizungumza na vyombo vya habari baada ya Kikao cha Makampuni hayo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.
……………………………………………………………..
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Makampuni ya Ulinzi Sekta Binafsi Tanzania ya yajipanga kuanzisha miradi ya maendeleo ili kuinua kipato chao.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Ulinzi Sekta Binafsi Tanzania Felix Kagisa leo baada ya Kikao cha Makampuni hayo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.
Kagisa amesema kuanzishwa kwa miradi mbalimbali kutasaidia makampuni hayo kusimama imara na kuweza kujiendesha bila utegemezi wowote.
Kagisa ametoa wito kwa makapuni ya ulinzi kwa kusema kuwa sasa ni wakati wa kufanya kazi ya ulinzi kama biashara ili kuongeza kipato chao kitakacho saidia uendeshaji wa makampuni yao bila changamoto.
“Lakini pia tumepanga kuanzisha mtandao wa kuorodhesha majina ya walinzi wote inchini ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi wa makampuni yote.
Aidha Kagisa amesema kuwa kila mlinzi atatakiwa kuwa na kitambulisho na lengo la kuanzisha mtandao huo nchini ni kuimarisha hutoaji wa huduma ya ulinzi nchini inakuwa imara.
“Baadhi ya makampuni yameshaanza kuandikisha majina ya walinzi wao ili kuwasilisha katika mtandao huo jambo litakalo saidia upatikanaji wa mlinzi pale panapotokea changamoto yoyote katika kituo chake cha kazi”, ameeleza Kagisa.
Pia Kagisa amesema kuwa wameandaa rasmu itakayowasilishwa bungeni na kujadiliwa ili kuweza kuwa na sharia itakayoongoza makapuni hayo katika hutoaji huduma hapa nchini.
Kagisa ameongeza kuwa sekta hiyo wamekutana kuweka mikakati ya kuweza kusukuma maendeleo ya utendaji wao na kuangalia changamoto zilizopo namna ya kuzitatua ili kuleta ubora katika utoaji huduma kwa jamii.
Vile vile Kagisa amesema kuwa walikuwa wanajiandaa na mkutano mkuu wa uchaguzi utakaofanyika mwakani mwezi wa Pili, kwani kila baada ya miaka mitano wanafanya uchaguzi wa viongozi wapya.
“Changamoto kubwa katika makapuni yetu hapa nchini ni kwamba wanatoza kiwango cha chini cha fedha na kufanya sekta hiyo kuwa imara na kuleta changamoto ndogo ndogo kwa watendaji”,ameeleza Kagisa.