Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na baadhi ya wakulima wa zao la korosho katika Wilaya ya Kibiti pamoja na viongozi wengine wa serikali pamoja na watendaji wa vyama vya ushirika wakati wa uzinduzi wa mnada wa kuuza zao hilo uliofanyika nje ya viwanja vya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kibiti.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wa kati kati akiwa ameshika korosho akiwa katika moja ya maghala ya kuhifadhia zao la korosho Wilaya ya Mkuranga kwa ajili ya kujionea shughuli mbali mabli ambazo zinafanywa na wataalamu wa kilimo katika kuzichambua ili kuweza kuzitofautisha ubora na kuziweka katika gredi mbali mbali.
Mwonekano wa baadhi ya wakulima wa zao la korosho kutoka Wilaya ya Kibiti pamoja na Rufiji aambao walifika kwa ajili ya kuweza kushuhudia halfa ya uzinduzi wa mnada maalumu kwa ajili ya kuuza zao la korosho.
Katibu Tawala msaidizi wa Mkoa wa Pwani Shangwe Twamala ambaye pia nashughulikia masuala ya uchumi akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kabla ya kuanza kwa zoezi la kufanya mnada huo amabo ulifanyika Wilayani Kibiti. Baadhi ya viongozi wa Chama kikuu cha ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU) wakiwa wanatoa ufafanuzi kwa wakulima ambao walifika katika zoezi la mnada huo jinsi ya taratibu zinazotakiwa kufanyika katika suala zima la kumpata mzabuni wa kununua korosho hizo.
****************************************
VICTOR MASANGU, KIBITI
SERIKALI mkoani Pwani imepiga marufuku vitendo vya baadhi ya wakulima kuchanganya zao la korosho na mawe kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha ubora unaotakiwa na pia haitowafumbia macho na kuwavumilia viongozi wa vyama vya ushiriika ambao watalihujumu zao hilo na kufanya ubadhilifu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea maghala ya kuhifadhia zo la korosho pamoja na kufanya uzinduzi rasmi wa mnada wa ununuzi wa zao la korosho awamu ya kwanza kwa msimu wa mwaka 2020/2012 ambao umefanyika katika viwanja vya Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Kibiti .
Katika halfa hiyo ya uzinduzi wa mnada wa kuuza zao la korosho ilihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo wakuu wa idara, pamoja na wakuu wa wilaya tano ambazo zinalima zao hilo ikiwemo Rufiji, Kibiti, Mkuranga, Kibaha pamoja na Wilaya ya Kisarawe.
Ndikilo alisema kwamba katika Mkoa wa Pwani zao la koroshi ni mkombozi mkubwa sana kwa walima kwani linaweza kuleta mabadiliko makubwa ya kukuza uchumi na kujiongezea kipato kwa wananchi hivyo serikjali itahakikisha kwamba inaweka mipango madhubuti ambayo itasaidia katika kuwajali wakulima katika maeneo mbali mbali.
“Leo hii ndugu zangu tupo katika mnada huu wa uuzaji wa zao la korosho lakini kitu kikubwa ninachowaomba ni kuhakikisha kwamba wakulima wote mnazingatia yale yote amabyo mnapatiwa na wataalamu wa kilimo kwa lengo la kuweka misingi mizuri ya kupata kurosho nzuri na zilizo na ubora ili kupata soko kwa urahisi sambamba na kufanya usafi katika mashamba yenu,”alisema Ndikilo.
Aidha alifafanua kuwa katika msimu serikali ya Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wataalamu mbali mbai wa kilimo waliweza kutoa elimu mbai mbai pamoja na kukutana na wadau mbali ili kuweza kujadili namna ya kufanya katika msimu huu mpya wa zao la korosho ili kuondokana na changamoto amabzo zimejitokeza katika kipindi cha nyuma.
“Hivi karibuni tuliweza kukutana pale Wilayani Mkuranga na wadau wa zao la korosho, viongozi mbali ma bli wa vyama vya msingi pamoja na wakuu wa idara lengo ilikuwa ni kuona namna ya kuweza kuboresha zaidi mwenendo mzima wa zao hili pamoja na kuona jinsi ya kutatua chanagmoto mbali mabli zinazowakabili wakulima na hili tulilifanya na kuna mambo tulikubaliana,”alifafanua Ndikilo.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa anasikitishwa sana kuona baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika kwenda kinyume kabisa na utaratibu uliowekwa kwa kuwanyonya wakulima wa zao hilo hali mabyo inawafanya washindwe kutimiza malengo amabyo wamejiwekea katika suala zima la kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.
Nao baadhi ya wakulima wa zao la korosho kutoka Wilaya ya Kibiti akiwemo Seif Njela na Jamal Amidu waliiomba serikali kuhakikisha inawasaidia upatikanaji maguni pamoja na maghala kwa ajili ya kuifadhia mazao yao sambamba na kuomba kupunguziwa gharama kwa ajili ya toza za usafirishaji ikiwepo kuwatafutia wanunuzi wa uhakika ambao watanunua kwa bei ya juu na sio kuwanyonya.
Awali Kwa upande wake Katibu Tawala msaidizi wa Mkoa wa Pwani Shangwe Twamala alibainisha kuwa katika msimu korosho zilizopo katika baadhi ya maghala ambazo zinatarajiwa kuuzwa ni zaidi ya tani elfu 3709.1 ambapo maghala makubwa matatu ya kibiti, Ikwiriri, na Mkuranga yanafanya kazi isipokuwa ghala moja la Wilaya ya Kibaha ambalo linakabiliwa na changamoto ya kuezuliwa na mvua.
Mkoa wa Pwani katika msimu huu mpya wa mwaka wa 2020/2021 umeweza kukusanya zao la korosho zaidi ya tani elfu 3000 ambapo katika mnada wa kwanza uliofanyika katika Wilaya ya Kibiti zao hilo limeweza kununuliwa kwa bei ya kiasi cha shilingi elfu 2153 kwa bei ya juu katika gredi ya kwanza huku gredi ya pili bado ikiwa hazijauzwa mpaka mnada mwingine wa pili utakaofanyika wiki ijayo.