Meneja wa EWURA Kanda ya Kati Mhandisi Norbert Kahyoza akifungua semina ya mafunzo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo,ili waweze kutambua haki zao za msingi kama watumiaji iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Meneja wa EWURA Kanda ya Kati Mhandisi Norbert Kahyoza akisisitiza jambo wakati wa semina watu wenye ulemavu wa ngozi iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo,yenye lengo la kuwapa elimu ili waweze kutambua haki zao za msingi kama watumiaji iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia Semina ya mafunzo kutoka kwa Meneja wa EWURA Kanda ya Kati Mhandisi Norbert Kahyoza, kwa watu wenye ulemavu wa ngozi iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo,ili kutambua haki zao za msingi kama watumiaji iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Taasisi ya kuongeza uelewa kwa jamii juu ya watu wenye ualbino(AAF), Suleiman Magoma, akiipongeza EWURA kwa kutoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambao utahamasisha ushiriki wa kundi hilo katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.
Meneja wa EWURA Kanda ya Kati Mhandisi Norbert Kahyoza akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina kwa watu wenye ulemavu wa ngozi iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo,ili waweze kutambua haki zao za msingi kama watumiaji iliyofanyika leo jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA), imetoa mafunzo ya uelimishaji kwa watu wenye ualbino kuwa mabalozi wa kutoa elimu kwa wenzao ili kusaidia kujua wajibu wa watoa huduma na watumiaji.
Akizungumza kwenye semina ya uelimishaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi yaliyoandaliwa Mamlaka hiyo jijini Dodoma Meneja wa EWURA Kanda ya Kati, Mhandisi Norbert Kahyoza, amesema kuwa yatasaidia kundi hilo kujenga uelewa kwa wengine na kuhakikisha wanatambua haki zao za msingi kwa watumiaji wote.
Hata hvyo amesema kuwa Kundi likasimame kama barozi wa huduma zao kwa umma uliobaki nje.
“Wito wetu kwenu ni mtakapoelewa EWURA ni nani na anafanya nini mtusaidie kueneza elimu hii kwa wengine ambao hawajapata bahati ya kuhudhuria mafunzo haya” ametoa wito Mhandisi Kahyoza.
Aidha ameeleza kuwa elimu hiyo itawasaidia kujua EWURA kwa kina, kuwa wanafanya nini na masuala ya leseni na kuadhibu mtoaji wa huduma anapokiuka matakwa ya leseni.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya kuongeza uelewa kwa jamii juu ya watu wenye ualbino(AAF), Selemani Magoma, amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhamasisha ushiriki wa kundi hilo katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.
“EWURA wametambua watu wenye ualbino kama wadau muhimu katika masuala ya kimaendeleo na kuona umuhimu wa kuwashirikisha katika kuwapa elimu kuhusu kazi na majukumu mbalimbali ya EWURA,”amesisitiza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa watu wenye ualbino Dodoma, Ludovick Julius, ameipongeza Mamlaka hiyo kwa kutoa elimu hiyo na kusema inamanufaa kwao na namna ya kutoa mapendekezo yao kama kuna tatizo kwa watoa huduma.