Wachezaji wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC wamerejea kambini kwa ajili ya kuendelea kufanya maandilizi ya Ligi kuu soka Tanzania Bara 2020/2021 ikiwa ni baada ya kupewa mapumziko ya siku nne mara baada ya kurejea kutoka Jijini Mwanza Novemba tano mwaka huu.
Aidha wachezaji ambao hawajarejea kikosini hadi sasa kwasababu mbalimbali ni pamoja na Juma Kaseja, David Brayson ambao waliitwa katika timu ya Taifa ,Taifa Stars ,Hassan Kapalata, Rahim Sheih, Israel Mwenda ambao waliitwa katika kikosi cha Timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes), pamoja na Keny Ally ambaye alifiwa na Baba yake mzazi.
Aidha wachezaji hao wamerejea wakiwa katika hali nzuri na kwamba utaratibu wa kuanza kufanya mazoezi unafanyika na hivyo wakati wowote kuanzia sasa wataanza kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Namungo utakaochezwa mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kimataifa.
“ Tumejipanga katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kwa muda ,tuna waandaa wachezaji wetu pindi tutakaporejea, tutahakikisha kuwa tunafanya vizuri katika michezo iliyopo mbele yetu tukianza na Namungo.