Baadhi ya wachezaji wa timu ya Lipuli iliyoshuka daraja kutoka ligi kuu hadi ligi daraja la kwanza ligi daraja la kwanza
Na Fredy Mgunda,Iringa.
UONGOZI wa timu ya mpira wa miguu ya Lipuli ya
mkoani Iringa umesema kuwa kushuka daraja kutoka ligi kuu Tanzania Bara hadi
ligi daraja la kwanza Tanzania Bara kuna changiwa na mlipuko wa virusi vya
ugonjwa wa Corona.
Akizungumza na blog hii katibu wa
timu hiyo ya Lipuli Jullias Leo alisema kuwa sababu za kushuka daraja inatokana
na kulipuka kwa ugonjwa wa Corona ambao ulisababisha kusimama kwa ligi kuu
Tanzania Bara na ligi nyingine nyingi duniani.
Alisema kuwa baada ya Corona
wachezaji wengi walirudi wakiwa wameongezeka uzito kutokana na wachezaji wengi
kutofanya mazoezi kwa wakati kutokana mpangilio maalum wa kocha wa timu.
Leo aliongeza kuwa baada ya Corona
timu hiyo ilishuka kiuchumi kutokana na wachangiaji wengi wa timu hiyo kushuka
kiuchumi kutokana na Corona na kusababisha kusuka kwa uchangiaji wa fedha kwa
wadau mbalimbali wa timu hiyo.
Alisema baada ya Corona wachezaji
muhimu wa timu hiyo kushindwa kurejea kambini kwenye timu hiyo kwa kuwa
walikuwa Wanamadai ya fedha ambayo yalishindwa kulipwa kutokana timu hiyo
kushuka kiuchumi.
Leo alisema kuwa kutokana na sababu
za Corona kocha wa timu hiyo ya Lipuli na baadhi ya wachezaji walishindwa
kurejea kambini kwenye timu hivyo kupelekea kuathiri mfumo wa uchezaji wa timu
kwa kuwa ili walazimu kutafuta kocha mwingine.
“Unapozungumzia mchezaji kama
Poul Nonga ndio alikuwa mfungaji bora wa timu yetu ya Lipuli hivyo baada ya
Corona timu ilikosa huduma ya mchezaji muhimu hivyo timu ilikuwa inashindwa
namna ya kufunga magoli mengi ambayo yangeisaidia timu yetu kubaki ligi
Tanzania Bara”alisema Leo
Nao baadhi ya wadau wa
mpira wa miguu mkoani Iringa Toshack Eliuter na Wiston kalumba walisema
kuwa kutokana na Corona uchumi kwa baadhi ya wapenda michezo washuka kiuchumi
na kusababisha kushindwa kuichangia timu na timu kushindwa kujiendesha
yenyewe.
Lakini pia waliongeza kuwa viongozi
wa timu ya Lipuli walishindwa kuandaa maandalizi mazuri ya timu hiyo na
kusababisha kuondoa kabisa mshikamano wa viongozi wa timu hiyo hadi pale
zilipobakia mechi tano za mwisho ndipo wakarudisha mshikamano wao lakini
walikuwa wamechelewa na kupelekea timu kushuka daraja kutoka ligi kuu Tanzania
Bara hadi ligi daraja la kwanza Tanzania Bara
Kwa upande wake mchezaji wa zamani wa
timu ya Costal Union inashiriki ligi kuu Tanzania Bara Hassan Ussi
alisema kuwa kutokana na Corona wachezaji wengi walishuka viwango na kushindwa
kufikia pale walipokuwa awali na kusababisha timu kama ya lipuli kushuka daraja
kutoka ligi kuu Tanzania Bara hadi ligi daraja la kwanza.
Alisema kuwa kutokana na Corona
uchumi kwa timu husika ulishuka na kupelekea timu kushindwa kutoa huduma bora
kwa wachezaji na wafanyakazi wa timu husika hivyo timu ambazo havina vyanzo
muhimu vya uchumi viliteteleka na kupelekea kushuka daraja.
Ussi alisema kuwa ili timu ifanye
vizuri kwenye mashindano lazima wachezaji wafanye mazoezi ya pamoja ili
kutengeneza uelewano wawapo uwanjani kwenye mechi za kishindani na kupata
matokeo mazuri
Naye daktari wa timu hiyo Dr Mwasabite
alisema kuwa mchezaji akiongezaka uzito lazima atapata majeraha ya mara kwa
mara kutokana na kutofanya mazoezi na baada ya janga la Corona lilipelekea wachezaji wengi kushindwa kurudi
kwenye viwango vyao kwa sababu ya kuongezaka uzito.