Kutana na Delvina Japhet Tarimo, mwenye umri wa miaka 31 aliyeweka record ya kuwa Mtanzania wa kwanza kumaliza Phd ya physics ndani ya mwaka mmoja na miezi sita katika Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini.
Study yake inahusu “Synthesis and characterization of a novel sulphuric-reduced graphene oxide/metal oxides composite for supercapacitor applications“.
Study hii imefanikiwa kutoa paper tatu ambazo zimekuwa published kwenye international journal zenye high impact factor 6.215 na 4.939 (Electrochemica acta na international journal of hydrogen energy).
Study hii ina muendelezo wa supercapacitor for commercial applications.
Pia katika umri wake huo mdogi ana shahada za masters mbili.
Kwa sasa CV ya Delvina inasomeka kama ifuatavyo:
PhD in Physics – University of Pretoria, South Africa
MSc. Physics – University of Dar es salam
M – Education
BSc. (Physics and Mathematics) – St. John’s University