Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha Kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha, Joram Mtafya (kushoto) akichagua kuponi wakati wa bahati nasibu ya mawakala wa konyagi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,(Kulia) ni Meneja Usimamizi wa kanda za Mauzo wa TDL, Mwesige Mchuruza.
Baadhi ya pikipiki za usambazaji ambazo mawakala wamejishindia.
Meneja wa kiwanda cha Konyagi, Aranyaeli Ayo (kulia) akikata utepe kuzindua mchezo wa bahati ya mawakala wa kampuni hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam ambapo wawakala 4 wamejishindia pikipiki za matairi 3,kushoto kwake ni Meneja Usimamizi wa kanda za Mauzo wa TDL, Mwesige Mchuruza.
……………………………………………………………………….
Mawakala wanne wa kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji maarufu cha Konyagi na jamii zake, wanaofanyia biashara zao katika mikoa mbalimbali nchini, wamejishindia pikipiki zenye magurudumu matatu za usambazaji kila mmoja baada ya kuibuka washindi katika kampeni ya mauzo ya miezi 3 ambayo ilikuwa inaendeshwa na kampuni kuanzia mwezi Julai mpaka Septemba mwaka huu.
Bahati nasibu ya kuwapata washindi ilifanyika katika kiwanda cha Konyagi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki chini ya usimamizi wa Bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha na kuhudhuriwa na na maofisa mbalimbali kutoka kampuni hiyo.
Akiongea wakati wa bahati nasibu hiyo,Meneja Usimamizi wa kanda za Mauzo wa TDL,Mwesige Mchuruza ,alisema kuwa kampeni hiyo iliyolenga kuwawezesha mawakala wa kampuni wanaouza kinywaji cha Konyagi imefanyika kwa kipindi cha miezi mitatu na mawakala 64 walifikia vigezo vya kuingia katika shindano ambapo miongoni mwao wanne wameshinda kupitia bahati nasibu na wamefanikiwa kujishindia pikipiki za kubeba mizigo.
Aliwataja mawakala walioibuka na ushindi kuwa ni Victoria Simba Ufoo (kanda ya kusini), Nkamba Zephania Masaladi- (Kanda ya Kaskazini Magharibi), Yatenga Company- (Nyanda za Kusini) na Agness Method Mtenga- (Kaskazini Mashariki).” Ni faraja yetu kubwa tukiona huduma za bidhaa zetu zikiboreshwa kila mara na kuwafanya wasambazaji wetu wawe na motisha ya kuendelea kufanya kazi na sisi tunawashukuru wote walioshiriki,” alisema Mchuruza.
Aliongeza kuwa kampeni hii ni mwendelezo wa kampeni za kampuni kupitia mpango wa kuwaendeleza wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa zake, mbali na kuwapatia zawadi vifaa vya kuwarahisishia usambaza pia imekuwa na utaratibu wa kuwapatia mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kukuza biashara zao.