……………………………………………………………………..
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Jumla ya Wanafunzi 646,148 wavulana wakiwa 301,831 sawa na asilimia 46.71 na wasichana 444, 317 sawa na 53.29% leo wameanza mtihani wa upimaji wa kidato cha pili mwaka 2020,
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Sekondari Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Benjamin Oganga wakati akitoa taarifa ya wanafunzi walioanza mitihani hiyo.
Aidha Oganga amesema wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanaofanya mtihani huo ni 731, uoni hafifu 406, wasioona 55, viziwi 3, na walemavu wa viungo 267 kati ya wote wanaofanya mtihani huo.
Oganga ameeleza kuwa Mwaka 2019 wanafunzi waliofanya mtihani wa upimaji wa kidato cha pili walikuwa 609, 502 tofauti na mwaka huu ambapo kuna ongezeko la wanafunzi kwa asilimia 5.7%.