******************************************
Na Ferdinand Shayo ,Arusha.
Chama cha Wakulima Tanganyika (TFA) kimewekeza kwenye Vifaa vya Kisasa na Wataalamu waliobobea katika upimaji wa afya ya udongo ambao tayari umeanza kuwapimia Wakulima udongo ili waweze kujua aina ya udongo na mazao wanayopaswa kulima na kupata mazao mengi hivyo kuinua uchumi wao.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi (TFA) ,Peter Sirikwa amesema kuwa wamejizatiti kuhakikisha kuwa wanawapimia wakulima udongo wao ili waweze kutambua aina ya pembejeo wanazoweza kutumia ikiwemo mbolea.
“Tuna vifaa vya kisasa na wataalamu wa kutosha tutaanza kupima afya ya udongo kwa wakulima waweze kujua kiasi cha rutuba kilichoko kwenye udongo na aina gani ya mbegu wanaweza kutumia” Alisema Sirikwa.
Naibu Gavana amepongeza juhudi za TFA na kuwataka kuongeza idadi ya wanachama ili waweze kuwafikia wakulima wengi Zaidi.
Aidha ameitaka TFA kushirikiana na taasisi za fedha pamoja na Beki ya Kilimo ili kuinua wakulima na kukuza uchumi kupitia kilimo.
Mkurugenzi amesema kuwa wana mpango wa kuwafikia wakulima wengi nchini na tayari wana vituo 17 vya kusambaza pembejeo na wana mpango wa kuongeza vituo vingine.