…………………………………………………………………….
Beki wa Kimatifa wa Kenya Joash Onyango ameinusuru Simba kuchapwa na watani zao Yanga baada ya kusawazisha bao dakika za lala salama na kufanya timu hizo kutoka sare ya kufungana 1-1 Mchezo uliopigwa katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza kilikuwa bora kwa Yanga na waliweza kupata bao kupitia kwa Mshambuliaji wao Michael Sarpong dakika ya 31 kwa mkwaju wa Penati baaada ya Tuisila Kisinda baada ya kuangushwa na Joash Onyango.
Hadi timu zinaenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko huku Simba wakionekana kuliandama lango la Yanga.
Mnamo dakikia ya 86 Joash Onyango aliwanyanyua mashabiki wa Simba akifunga bao kwa kichwa akimalizia kona iliyopigwa na Luis Miqussone.
Mpaka dakika 90 zinamalizika watani wa jadi wameweza kugawana pointi moja moja kwa matokeo hayo Yanga wanabaki na Pointi 24 nafasi ya pili huku Simba wakifikisha pointi 20 nafasi ya tatu na Azam FC bado anaongoza Ligi kwa kuwa na Pointi 25.