TIMU ya Azam FC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Aggrey Morris dakika ya 47, kiungo mshambuliaji Ayoub Lyanga dakika ya 58 na beki Hassan Kapona aliyejifunga akijaribu kuokoa krosi ya kiungo Never Tigere dakika ya 62.
Kwa ushindi huo, Azam FC imfikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 10, sasa ikiwazidi ponti mbili , Yanga SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.