Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Injili mkoani Tabora Askofu Peter Shani akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu mkutano huo utakaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 15 Mwezi huu mjini humo.
NA TIGANYA VINCENT
WATANZANIA wamepomgezwa kwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID -19) ambapo wameweza kuushinda na kuufanya utoweke nchini humo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwinjilisti na Mkurugenzi wa maandalizi ya Mkutano mkubwa wa Injili Randy Roberts wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tabora.
Alisema Watanzania wakiongoizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wamefanikiwa kuondoa tatizo hilo na kuwawezesha kuendelea na shughuli mbalimbali.
“Watanzania hawakukubali kuupigia magoti ugonjwa wa COVID 19 badala yake walimuinua Mungu juu na hatimaye wamefanikiwa kuushinda …hongreni sana” alisema.
Alisema hali hiyo imewawezesha kuendelea kwa shughuli zinawaunganisha watu pamoja ikiwemo mikutano ya Injili na shughuli nyingine za Ibada.
Roberts alisema kutokana na uwepo wa mazingira salama nchini Tanzania wanatarajia kuendesha Mkutano Mkubwa wa Injili mkoani Tabora kuanzia wiki ijayo kwa ajili ya kuendelea kuwaombea watu wenye matatizo mbalimbali.
Mkurugenzi huyo alisema katika baadhi ya Nchi za jirani na Tanzania wameshindwa kuendesha mikutano ya Injili kutokana na kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID -19)
Alisema ndani ya wiki mbili zijazo wanatarajia kuwa na mikutano ya Injili katika maeneo ya Singida , Arusha, Shinyanga, Tabora na Kahama ambapo Mwinjilisti Jared Horthon ataongoza katika kuwaombea wakazi wa maeneo hayo