Warembo 20 kutoka Kanda 5 za mikoa ya Tanzania wanatarajia kuanza kambi ya mchuano wa Fainali za Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania tarehe 26 Novemba 2020 jijini D’salaam.
Hatua za awali za mashindano haya ulianza mapema mwezi Februari mwaka huu, baadae mchakato ulisitishwa kidogo kutokana na janga la ugonjwa wa Corona ulioikumba nchi yetu pamoja na dunia kwa ujumla.
Mchakato wa kuwapata washiriki 100 wa awali uliendelea mwezi Juni mara baada ya tishio la ugonjwa wa virus vya Corona kumalizika, ambapo mchujo wa washiriki 100 ulifanyika na kuwapunguza hadi washiriki 50.
Washiriki 50 walipewa majukumu ya kufanya na kuwasilisha majibu yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania ambao ndio walikuwa na jukumu la kudadisi na kuperuzi majibu ya washiriki wote.
Kati ya washiriki 50 ni washiriki 20 tu ndio waliopita katika mchakato huo, nao wameshajulishwa tayari kuhusu kuingia kambi ya Miss Tanzania mwisho wa mwezi Novemba.
Majina ya washiriki hao pamoja na umri wao ni kama ifuatavyo:-
- PRISCA LYIMO umri miaka 22
- TAMIA HAKAM miaka 19
- JULIANA RUGUMISA miaka 23
- REHEMA CUTHBERT miaka 21
- YVONNE PAUL miaka 20
- RUTH BENITHO miaka 23
- GRACE MACHIBULA miaka 24
- ROSE MANFERE miaka 20
- MARGARET MWAMBI miaka 23
- SARAFINA MAGEYE miaka 20
- MARTHA GOLODI miaka 23
- ZENITHA CHUNDU miaka 22
- DEOLYN MOLLEL miaka 21
- HOYCE BAKANOBA miaka 20
- NECERIAN KIVUYO miaka 20
- RAZIA ABRAHAM miaka 19
- ANGELA PENDAELI miaka 23
- ADVERA MWEMBA miaka 21
- VERYNICE DEOKARI miaka 24
- GLORIA FELA miaka 23
Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania yanaandaliwa na Kampuni ya The Look chini ya Mkurugenzi wake Bi. Basilla Mwanukuzi Shayo. Miss Tanzania 1998.