Kesho Novemba 5, 2020, jijini Dodoma, Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anatarajia kuapishwa rasmi baada ya kushinda uchaguzi wa Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika 28 Oktoba 2020.
Marais watano watahudhuria huku viongozi wa mataifa yaliyobakia yatawakilishwa na mawaziri na mabalozi wao waliopo nchini.
Aidha, viongozi wa jumuiya za kikanda na za kimataifa nao watashiriki katika sherehe hizo.
Dkt. Magufuli alishinda kwa kupata kura 12,516,252 sawa na asilimia 84.4 ya kura halali.