NGOMA AFRICA BAND YA UJERUMANI YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA TENA
Bendi maarufu ya muzuki wa dansi barani ulaya The Ngoma Africa Band almaarufu FFU-Ughaibuni yenya makao yake nchini ujerumani inaipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa tena kuingoza jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kipindi miaka mitano tena.kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja alitoa pongezi hizo kwa niaba ya bendi yake alipokuwa akiongea studio za media City ziliopo katika mji wa Amsterdam,Holland ambako alikuwa akifanya ziara fupi ya vyombo vya habari nchini Uholanzi.
Kamanda Ras Makunja amewapongeza wa Tanzania kwa kupiga kura kwa amani na kuonyesha mfano bora utakauigwa na nchi zingine za kiafrika,Tanzania imeionyeshea dunia kwa kufanya uchaguzi kwa kutegemea za pesa zake za ndani mwanamziki huyo alisisitiza.
Ras Makunja amewaomba watanzania wanaoishi nyumbani na nje ya Tanzania kushiriki katika ujenzi wa Tanzania wa viwanda na uchumi,pia kuitunza amani ya tanzania daima milele.bendi hiyo inaendelea kutamba na CD ya “Awamu Ya Tano Uwanjani”