Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na Maandalizi kwa ajili ya kuampisha Rais Mteule wa Tanzania kesho jijini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge wakati akitoa taarifa Ofisini kwake kuhusiana na Maandalizi kwa ajili ya kuampisha Rais Mteule wa Tanzania.
………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
MAANDALIZI ya uwanja wa Jamhuri Dodoma kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule John Magufuli yamekamilika kwa huku wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia tukio hilo la kihistoria kwa Mkoa wa Dodoma
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na Maandalizi yalivyokamilika kwa ajili ya kuampisha Rais Mteule wa Tanzania.
Aidha amesema kuwa maandalizi ya sherehe hizo yamefanyika kwa kutumia fedha za ndani jambo ambalo ni matokea ya Rais ya kukusanya kodi.
Dkt. Mahenge amesema kuwa Rais Magufuli ataapishwa jijini Dodoma ambapo itawekwa historia ambapo kwa mara ya kwanza rais kuapishwa nje ya jiji la Dar es salaam.
“Tukiwa tunaingia katika historia tangu kupata uhuru kwa mara ya kwanza sherehe hizi zitafanyika Dodoma na siyo Dar es salaam kama ilivyo zoeleka”amesema
Dkt.Mahenge ametumia fursa hiyo kuwataka wanadodoma na wananchi wote kwa ujumla kutoka mikoa mbalimbali kuhudhuria kwa winginkatika shughuli hiyo