…………………………………………………………………………………………..
KMC FC Kikosi cha Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kimewasili leo hii jijini Dar es Salaam kikitokea jijjini Mwanza ambapo kilikuwa huko kwa muda wa siku 14 kwa ajili michezo mbalimbali ya ligi kuu Soka Tanzania bara 2020/2021.
Kikosi hicho cha wana Kino Boys kiliondoka Oktoba 22 kuelekea jijini mwanza kwa ajili ya michezo mitatu ambayo ni KMC FC dhidi ya Yanga, Gwambi pamoja na Biashara ambapo imeweze kuondoka na alama nne katika michezo mitatu iliyochezwa kanda ya Ziwa.
Aidha mara baada ya kurejea jijini Dar es Salaam, wachezaji hao wamepewa mapumziko ya siku nne na hivyo kurejea kambini siku ya jumapili kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya michezo inayofuata ikiwa ni baada ya kumalizika kwa mapumziko ya mechi za kimataifa kwa muda wa wiki mbili.
Ikiwa kanda ya ziwa, KMC FC iliweza kupata matokeo ya ushidi ugenini dhidi ya Gwambina ambapo iliibuka na ushindi wa goli tatu kwa bila mchezo ulipigwa Oktoba 30 katika uwanjwa wa Gwambina Complex Misungwi ,kutoka zare dhidi ya Biashara ya Musoma mkoani Mara katika uwanja wa Karume mchezo uliopigwa hapo jana Novemba tatu.
Mbali na matokeo hayo, pia KMC FC iliweza kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Yanga ambao ulipigwa Oktoba 25 katika dimba la CCM Kirumba kwa kufungwa magoli mawili kwa moja huku ikiwa ni wenyeji wa mchezo huo.
KMC FC inakwenda katika mapumziko ya Ligi kuu ikiwa imeshacheza michezo 10 na kukusanya alama 15 huku ikiwa katika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu Soka Tanzania bara 2020/2021.