Mmoja wa wagonjwa wa kisukari ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando baada ya kukatwa miguu yote kutokana na kusumbuliwa na maradhi hayo, Ali Amani, mkazi wa Kisesa wilayani Magu, akiwa amekaa kwenye baiskeli aliyokabidhiwa na taasisi ya The Desk & Chair Foundation jana huku Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Alhaji Sibtain Meghjee wa tatu kushoto na Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Hospitali hiyo ya Kanda, Fr. Engelbert Nyandwi wakishuhudia.
Wafanyakazi wa The Desk & Chair Foundation wakishusha baiskeli za wagonjwa kutoka kwenye gari kabla ya kuzikabidhi kwa uongozi wa Hospitali ya Sekou Toure jana.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure, Dk. Bahati Msaki (kushoto) akipokea msaada wa baiskeli 15 za wagonjwa kutoka kwa Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Tawi la Tanzania, Alihai Sibtain Meghjee, kulia jana.Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Tawi la Tanzania, Ahaji Sibtain Meghjee, kushoto akimkabidhi msaada wa baiskeli 15 za wagonjwa, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC)Fr. Engelbert Nyandwi (kulia) jana.
Baiskeli hizo 30 zenye thamani ya 6.5 zimetolewa na taasisi hiyo kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa kwenye hospitali hizo kila moja ikipata 15 ambazo zitawezesha kukabiliana na uhaba wa vifaa hivyo kwa wagonjwa wenye mahitaji ikiwa ni maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W.
Akikabidhi msaada huo jana kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation,Tawi la Tanzania,Sibtain Meghjee, alisema walipokea jumla ya baiskeli 54 zenye thamani ya sh. milioni 20 zimetolewa na Waislamu wa Shia Ithna-sheria Imamia kwa matumizi ya wagonjwa waliolazwa wodini,wazee na watoto wenye mahitaji wasiojiweza waliopo nyumbani.
Alisema msaada huo wa baiskeli ambazo wamezisambaza kwenye Zahanati ya Kijiji cha Bugisi 10 mkoani Shinyanga,mkoani Mwanza Hospitali ya Bugando imepata 15 na Sekou Toure 15 huku mkoani Mara wakipata 6 na 8 kwa wazee na watoto wenye mahitaji ni zawadi kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa wakati wa maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad S.A.W duniani .
Meghjee aliupongeza uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya na uongozi wa hospitali za Bugando na Sekou Toure,wafanyakazi,madaktari na wauguzi kwa kazi kubwa ya kuwahudumia wananchi.
Alisema baiskeli zilizopo ni chache kulinganisha na idadi ya wagonjwa 1,200 hadi 1,500 wanaowapokelewa na kuwahudumiwa kwa siku ambapo nusu yao wanahitaji baiskeli hizo ili kurahisisha usafiri wao hospitalini hapo.
“Tunashukuru kwa msaada wa baiskeli hizi zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 6 kwenye hospitali yetu, namba inaongezeka kutokana na ubora wa huduma zinazotolewa na kwenye hospitali yetu ya Bugando na baiskeli hizi zipo chache ingawa hizi 15 zitapunguza changamoto,” alisema Fr. Nyandwi.
Aliongeza mchango wa The Desk & Chair Foundation na moyo wao wa kujitolea unatambuliwa na hospitali hiyo,imekuwa ikiwasaidia wagonjwa wasio na uwezo kulipia gharama za matibabu na kuwaombea walipotoa Mungu awajazie mara dufu.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure, Dk. Msaki alisema mbali na baiskeli hizo 15 wamenufaika na misaada ya The Desk & Chair Foundation,imechimba kisima kirefu cha maji,imeweka matenki, mfumo wa kusambaza maji,imejenga jengo la mionzi (CT Scan),vyoo matundu 20 na banda la kupumzikia wageni.
Alisema msaada huo umewarahisishia kufanya kazi kwa wepesi na kuomba iendelee kusaidia jamii ambapo kabla walikuwa na wheelchair 20 ambazo zilikuwa haziwiani na mahitaji ya wagonjwa kwani kwa siku wanapokelewa 500 hadi 700 mbali na waliopo wodini ambao huhitaji kushushwa kwenye vipimo na kurejeshwa