************************************
Kwa asiyejua kilichojificha nyuma ya pazia yano #Demokrasia anaweza kudhani ni uwanja sawa wa kisiasa unaowezesha watu kushiriki shughuli za kisiasa kupitia vyama kushindanisha sera, hoja na Ilani za vyama vyao ili kuaminiwa, kupigiwa kura na kuchaguliwa kwa viongozi kushika madaraka kwa njia ya kidemokrasia.
Lakini ukweli ni kwamba, duniani kuna mifumo miwili ambayo inashindana kila mfumo ukitaka kuitawala dunia kupitia kunadi sera zake, ikiwemo kuwaweka madarakani viongozi wenye kulinda maslahi ya mifumo hiyo. Mifumo hiyo ni Ubepari na Ujamaa (Ukomunisti au Usoshalisti). Mfumo wa Ubepari asili yake ni nchi za Magharibi na mfumo wa Ujamaa au Ukomunisti na Usoshalisti ni nchi za Madhariki.
#UBEPARI: Huu ni aina ya mfumo wa uchumi unaowawezesha kundi la watu wachache kuhodhi na kumiliki njia kuu za uchumi huku kundi kubwa la watu likibakia masikini na kutumikishwa kama vibarua na kundi la wachache. Kwenye mfumo huu, kati ya rasilimali zinazomilikiwa na wachache ni pamoja na ardhi.
#UJAMAA: Huu ni aina ya mfumo wa kiuchumi unaowezesha njia kuu za kiuchumi ikiwemo ardhi, viwanda, mashirika ya uzalishaji mali, taasisi za fedha ikiwemo mabenki kumilikiwa na umma kwa maslahi ya wengi, na faida inayopatikana hugawanywa na kutumika kupitia huduma za kijamii kama vile afya, elimu, maji, umeme na ujenzi wa miundombinu. Mfumo huu hutumika zaidi kwenye nchi zenye kufuata sera ya haki sawa kwa wote ikiwemo Tanzania.
#UJIO_WA_DEMOKRASIA_NA_MALENGO_YAKE:
Huko nyuma mfumo wa utawala uliofuata siasa za Ujamaa au Kikomunisti ulionekana kutokuwa na utaratibu wa viongozi kuachia madaraka au kupokezana nafasi za juu za uongozi baada ya mihula fulani kwa kiongozi kukaa madarakani. Kwa msingi huo, sehemu kubwa ya viongozi walioshika madaraka hawakuweza kuondoka kwa hiyari yao hadi kifo kitokee.
Kilichotokea ni kwamba, kuwepo kwa mfumo wa Kijamaa au Kisoshalisti duniani kulizinyima fursa nchi zenye kufuata mifumo ya kibepari kuweza kupata mwanya wa kunyonya rasilimali za kiuchumi kutoka nchi za kijamaa na kikomunisti ikiwemo madini na mali ghafi za viwandani.
Kwa msingi huo, demokrasia ya mfumo wa vyama vingi iliyopo duniani kwa sasa ilibuniwa na nchi za Magharibi kwa lengo la kufadhiri na kupandikiza viongozi vibaraka madarakani kwenye nchi zenye rasilimali kupitia uchaguzi wa kidemokrasia, huku lengo na madhumuni likiwa kurahisisha uchotwaji wa rasilimali hizo kupitia viongozi walionunuliwa walioko madarakani.
Hii ni baada ya kutambua kwamba, kupitia mfumo wa Kijamaa na Kikomunisti, isingewezekana kupata viongozi vibaraka na pandikizi watakaoruhusu rasilimali za nchi kunyonywa kurahisi.
#DEMOKRASIA_INAPOSHINDWA_NINI_HUFANYIKA?
Mfumo huu wa mataifa makubwa yenye nguvu za kiuchumi duniani, kupandikiza viongozi vibaraka madarakani kwa lengo la kuwatumia kunyonya rasilimali za mataifa yao, umekuwepo kwa kipindi kirefu, ambapo katika baadhi ya nchi umeshindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa kutokana na misimamo na uzalendo wa viongozi na wananchi wa nchi husika, na hivyo mabeberu wameanza kutumia mbinu nyingine mbadala, kama vile kufadhiri na kuchochea wananchi kutotii sheria za nchi na kuhasi serikali za nchi zao kwa kufanya maandamano, fujo, vurugu, uharibifu wa mali, ili nchi isitawalike, na hali hiyo inapotokea, mataifa hayo huingilia kati kuunga mkono wenye kuandamana kwa kisingizio cha kulinda demokrasia, uhuru wa kujieleza pamoja na haki za binadamu.
Hicho ndicho kilichotokea nchini Iraq, Libya, Tunisia, Syria, Misri, na sasa Iran na Venezuela. Suala la demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa kujieleza ni agenda inayotumiwa na mataifa makubwa ili kufikia malengo yao.
Mbinu hii ya kuwatumia viongozi vibaraka kuwapandikiza madarakani inaposhindwa kuzaa matunda, hatua inagofuata ni kutafuta kisingizio cha kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi husika hadi pale itakaposalimu amri. Miongoni mwa nchi zilizokumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na Zimbabwe, Cuba na Venezuela.
Hivyo ndivyo Marekani na washirika wake nchi za Jumuiya ya Ulaya zinavyofanya dhidi ya nchi zenye rasilimali kwa lengo la kujinufaisha na rasilimali za nchi masikini ikiwemo Tanzania, ambapo Tundu Lissu, Zitto Kabwe na Seif Sharif Hamad ni kati ya vibaraka waliokwisha ingia kwenye rada za mataifa hayo, na wako tayari kufanya lolote baya kwa nchi yao ili kutimiza lengo lililokusudiwa ikiwemo kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja, wanafunzi wa kike kuruhusiwa kubeba mimba wakiwa bado shuleni.
Unapoona mataifa ya Ulaya na Marekani yakiingilia mambo ya ndani ya mataifa mengine kwa kisingizio cha kudumisha haki za binadsmu, demokrasia, na uhuru wa kujieleza, hayafanyi hivyo kwa nchi masikini zisizo na rasilimali bali yanaangaika na mataifa yenye rasilimali za kiuchumi kwa ajili ya mataifa yao kama vile mafuta, madini na mali ghafi ya mazao kwa ajili ya uchumi wa viwanda vyao.
#FUNDISHO_KWETU_WATANZANIA:
Pamoja na kwamba ni hulka ya binadamu kutojifunza siku zote kutokana na makosa ya mwenzake mpaka yamkute mwenyewe ni muhimu kwetu sisi watanzania kujifunza na kuzibaini mbinu mbali mbali chafu zinazotumiwa na mabeberu kupandikiza viongozi vibaraka mfano wa Tundu Lissu, Zitto Kabwe, na Seif Sharif Hamad wanaotafuta madaraka ikibidi hata kwa njia ya kumwaga damu ili wafikie malengo waliyotumwa na mabwana zao.
Tunachotakiwa kufanya, licha ya kuwepo mfumo wa kisiasa wa kidemokrasia unaoruhusu viongozi vibaraka kugombea kupitia vyama vya siasa vinavyofadhiriwa na mabeberu, ni kutoruhusu viongozi wa aina hiyo kupata nafasi ya kuongoza mataifa yetu.
Kamwe tusiruhusu wala kukubali kiongozi kibaraka mwenye kushirikiana na mabeberu, iwe kupitia siasa au harakati za kijamii, kwa malengo hasi kwa nchi yetu kujiinua na kustawi ka walivyojiinua Jonas Savimbi wa Angola, Rieck Machar wa Sudan kusini na wengineo.
Amani, utulivu, umoja na mshikamano wetu ni muhimu zaidi kuliko maslahi ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache.