………………………………………………………………………………
Wanafunzi sita wa Kitanzania kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamefuzu kushiriki shindano la Huawei la TEHAMA Duniani baada ya kufanya vizuri katika fainali za Mashindano ya TEHAMA ya Kusini mwa Jangwa la Sahara ya Huawei. hafla ya utoaji Tuzo kwa washindi ilifanyika Mtandaoni siku ya jana Oktoba 29, 2020.
Shindano hilo linalenga kutoa jukwaa kwa vijana wenye vipaji kwenye TEHAMA kuonyesha uwezo wao, kushindana na kuwasiliana, kuhimiza utafiti wa TEHAMA, na kusaidia ukuaji wa mfumo thabiti wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Timu 13 zilizoshinda ni timu kutoka Tanzania, Uganda, Nigeria, Afrika Kusini, Kenya, Lesotho, Mauritius, Zambia. Timu hizo zitashindana na timu kutoka mabara mengine ikiwemo Marekani katika mashindano ya dunia Mwezi Novemba.
Miongoni mwa timu zilizopewa tuzo kwenye hafla hiyo ni timu 10 zilizoshiriki upande wa Network Track zikiwemo timu kutoka Tanzania, Uganda, Nigeria, Afrika Kusini, Kenya na Lesotho. Timu hizo zitaenda kushiriki mashindano ya Dunia baada ya kuchuana vikali kupata wawakilishi kwa kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara. Timu za Nigeria, Mauritius na Zambia zenyewe zilishinda upande wa Cloud Track.
Timu ya Tanzania ilikuwa na wanafunzi 9 ambao waligawanyishwa katika timu tatu. Timu mbili kati ya hizo zimefanikiwa kufika kwenye fainali za dunia, timu ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kati ya Zaidi ya timu 40 zilizoshiriki, na timu nyingine ilishika nafasi ya 4 na hivyo kupata nafasi ya kushiriki fainali za dunia.
Timu hizo zimeundwa na wanafunzi wa Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (COICT) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Washindi wa nafasi ya kwanza ni Mpoki Abel Mwaisela, Hongo Kelvin and Henry Kihanga na washindi wa pili ni Aghatus Biro, John Lazaro na Elisante Akaro.
Hafla hiyo ya utoaji tuzo imeashiria miaka mitano mfululizo ya kushiriki kikamilifu Shindano la TEHAMA la Huawei kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, shindano hilo limekuwa likivutia zaidi ya wanafunzi 50,000 kutoka nchi 14 za Afrika yakiwa na Kauli mbiu ya “Connection, Glory and the Future” na Uelewa mpya kuhusu TEHAMA kama vile Cloud computing, AI, mitandao ya simu na intaneti.
Katika hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyohudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu serikalini, viongozi wa tasnia, na wanafunzi, Makamu wa Rais wa Huawei Afrika Mashariki na Kati, Hou Tao aliangazia shauku ya wanafunzi kujifunza, ambayo inahitajika sana ili kuhakikisha mifumo ya Kidijiti inafika Afrika nzima katika zama ambazo ujuzi wa mahali pa kazi tayari unahamia mtandaoni.
Uzoefu wa kimataifa unaonyesha kuwa hili ni eneo muhimu ambapo ushirikiano wa umma na taasisi binafsi unaweza kuwa na mchango mkubwa. “Bwana Hou anasema,” Kama kampuni ya binafsi inayohudumia soko la Afrika kwa zaidi ya miaka 20, Huawei imejitolea na itabaki kuwa mshirika wa kuaminika wa serikali na taaluma katika kujenga vipaji na wanataaluma wa TEHAMA, kuimarisha uwezo na kuongeza uwezo wa watu wa dijiti. . ”
Akiongea kama mwakilishi wa waalimu wa Chuo Kikuu, Prof.Funso Falade, Rais wa Jumuiya ya Elimu ya Uhandisi Afrika (AEEA) aligusiachangamoto kadhaa dhidi ya mafunzo ya wahandisi barani Afrika kama ufadhili, kuchoka kwa akili, na ushirikiano dhaifu wa vyuo vikuu / tasnia. Pia alisifu jitihada zinazofanywa na Huawei katika kukabiliana na changamoto hizi.
“Fursa za kukuza ujuzi zinazotolewa na Kampuni ya Huawei zinaambatana na lengo na matarajio ya AEEA kwa wanafunzi wetu na eneo muhimu ambapo sasa tunahitaji utaalam mwingi barani Afrika kuliko wakati wowote kabla, hasa ukizingatia changamoto zilizoletwa na janga la COVID-19 kwenye mfumo wetu wa elimu, ”aliongeza.
Shindano la TEHAMA la Huawei ni moja ya tukio kubwa la aina yake. Miongoni mwa nchi zinazoshiriki, Zambia, Kenya, Tanzania, na Afrika Kusini zilifanya sherehe ya ufunguzi wa kitaifa au tuzo ambapo mawaziri na maafisa wengi katika sayansi na elimu walizungumza kupongeza kazi inayofanywa na Shindano hilo na mchango wa Huawei katika kukuza vipaji vya Sayansi na teknolojia Afrika.