Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani anayemaliza muda wake Job Ndugai akichukua fomu ya kuwania tena nafasi hiyo katika Bunge lijalo la 12 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake Dkt. Tulia Ackson akichukua fomu ya kuwania tena nafasi hiyo katika Bunge lijalo la 12 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Makao Makuu ya CCM Dodoma.
………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Baada ya kutoka taarifa kwa wanachama wa CCM kuomba dhamana ya Spika na Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani hatimaye leo Spika anayemaliza muda wake Job Ndugai pamoja na Naibu wake Dkt. Tulia Akson wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Spika na Naibu Spika katika ofisi za CCM Taifa jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Katibu Mkuu Msaidizi wa Oganaizesheni CCM Taifa Solomon Itunda, amesema kuwa zoezi hilo limefanyika kwa kufuata taratibu zote.
Itunda amemtaja Spika anayemaliza muda wake ambaye pia ni Mbunge Mteule wa Kongwa Job Ndugai na Naibu spika anayemaliza muda wake Mbunge mteule wa Mbeya mjini) Dk.Tulia Akson kuwa ndio wagombea pekee wa nafasi hiyo ambao wamejitokeza na kukamilisha taratibu zote.
Itunda amesema kuwa Job Ndugai amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Spika huku Dk.Tulia akichukua fomu kuwania nafasi ya Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hata hibyo amesema kuwa gharama za fomu kuwa ni shilingi laki tano za kitanzania kwa kila fomu.
Kwa upande wake Job Ndugai mara baada ya kukamilisha taratibu zote za kujaza na kurejesha fomu amesema kuwa anawaomba watanzania kumuombea ili Chama chake kimteue kwa mara nyingine kugombea nafasi hiyo.
Aidha Ndugai amesema kuwa nafasi ya Spika inapendekezwa na vyama vya siasa hivyo ikiwa chama chake kitamkubalia Kuwa spika wa bunge la 12 wataongea na watanzania kwa Wakati huo juu ya Vipaumbele vyao.
Naye Dk.Tulia Akson amesema kuwa yeye kwa ridhaa yake ameamua kuchukua fomu kuwania kiti Cha Naibu spika huku akieleza kusukumwa kufanya hivyo Kutokana na kubanwa na majukumu.
“Nimechaguliwa kuwaongoza Wananchi wa Mbeya mjini hivyo majukumu yatanibana Sana nikigombea nafasi ya uspika hivyo kwa nafasi hii itatosha kabisa kuwatumikia watanzania,”amesema Dkt.Ndugai