*****************************************
Umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) umesema uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 27-28, mwaka huu ulikua halali.
Aidha, NAM imelaani vikali kitendo cha Marekani kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania.
Umoja huo unaundwa na mataifa 120 yanayoendelea ulianzishwa kupitia Azimio la Havana la mwaka 1979 na kwamba ndio chombo kikubwa ulimwenguni baada ya Umoja wa Mataifa.
Lengo la kuanzishwa umoja huo ni kuhakikisha “Uhuru wa kitaifa, mamlaka kamili, kuheshimu mipaka na usalama wa nchi zisizofungamana na upande wowote”.
NAM pia inaunga mkono mapambano dhidi ya ubeberu, ukoloni, ukoloni-mamboleo, ubaguzi wa rangi, na aina zote aina zote za uchokozi wa mataifa ya kigeni.