WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA)Mhandisi Victor Seff wakati wa ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba iliyofanyika leo jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,akiwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba iliyofanyika leo jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,akitoa maelezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya China Hainan International Cooparation (CHICO) ambaye anajenga barabara za Mji wa Serikali Mtumba iliyofanyika leo jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,akiangalia ramani ya mchoro wa ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba iliyofanyika leo jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,akitoa maelekezo kwa Mkandarasi mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Muonekano wa ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Muonekano wa jengo la hospitali ya Uhuru lililopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,akisikiliza taarifa kutoka kwa Msanifu wa ujenzi wa SUMA JKT Girimu Kanansi alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali ya Uhuru wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Uhuru iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akimpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya hivyo anaimani kuwa atarudi katika Wizara hiyo.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali ya Uhuru iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma
…………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,amesema kuwa hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara za mji wa serikali Mtumba.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo huku akimtaka mkandarasi wa kampuni ya China Hainan International Cooparation (CHICO) kutotumia kigezo cha Covid 19 kama sababu ya kutokamilisha kazi hiyo kwa wakati.
”Kiukweli sijaridhishwa na kasi ya ujenzi unavyoendelea hivyo nakutaka mkandarasi ulete vifaa vyote vya kazi vinavyohitajika ili kazi ziende haraka na kukamilika kwa wakati”amesema Jafo
Jafo amesema kuwa Mkataba unataka kazi hii ikamilike Julai 2021 naomba iwe hivyo hakuna justification ya Covid tunaelekea kwenye msimu wa mvua unavyoenda, Disemba ni kipindi cha mvua sasa mkilegalega hapa huko mbele itakuwaje.
”Mkandarasi usilete ubishororo hapa nikiangalia kazi haiishi,malizeni kazi tena kwa kiwango kinachotakiwa kitaalam,sio barabara inajengwa leo muda mfupi lami inavimba hapana,”amesisitiza
Naye Mtendaji mkuu wa wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amesema kuwa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 40 inajengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Sh Bilioni 88.1 na imefanikiwa kutoa ajira 240.
Mhandisi Seff amesema kuwa Mradi huu ulianza rasmi Februari mwaka huu na unategemewa kukamilika julai 2021.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo amekagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Uhuru iliyopo wilayani Chamwino Dodoma na kuridhishwa na ujenzi huo huku akiomba kuwa ukamilike kwa wakati ili dhamira ya Rais Dkt Magufuli iweze kutimia.
“Leo nimekuja kukagua hapa na binafsi naona kazi inaendelea vizuri,ila changamoto ninayoiona hapa ilikuwa kuchelewa kwa upatikanaji wa material,lakini nafurahi kuwa changamoto hiyo imetatuliwa na kiasi cha Sh Bilioni 1.2 kimeletwa ili kumalizia kazihii,hivyo hakuna sababu ya kutokamilika,kazi iendelee na Disemba 5 ikamilike,”amesema
Kwa upande wake Msanifu ujenzi wa SUMA JKT Girimu Kanansi amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Sh Bilioni 3.99 ambapo ujenzi kwa sasa umefikia asilimia 90.