************************************
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Iringa Mjini, Salvatory Ngelela amewataka vijana mkoani hapa kupuuzia maandamano ambayo yametangazwa na vyama pinzani ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu kwamba hayana tija kwa sasa.
Akizungumza na wanahabari mkoani hapa,Ngelela alisema kuwa vijana mkoani hapa wamemtuma kusema hayo kwa kuwa wamejadili hakutakuwa na maandamano kutokana na sababu mbalimbali walizotoa.
Alisema kuwa sababu kubwa ambayo hawataandamana ni ajenda ya tume huru ya uchaguzi wanayoizungumzia wapinzani huwa inakuja Mara tu baada ya chadema kushindwa katika uchaguzi.
Alisema kuwa ikumbukwe mwaka 2015 ilikuwa kipindi kigumu sana kwa CCM ambapo kilipoteza viti vingi vya ubunge kwa chadema na tume hiyo hiyo iliyotangaza ushindi wa chadema kwa viti 70 vya ubunge lakini hakulalamikiwa kwamba sio huru lakini iweje leo wameshindwa wanaleta hoja za tume huru?
Alisema kwa kuuliza tume hiyo hiyo mwaka huu imekuwa sio huru baada ya CCM kushinda? Basi maswali hayo yaelekezwe kwa hao wanaohoji kuhusu tume huru ya uchaguzi na kuratibu maandamano.
Alisema kuwa sababu ya pili ni kuhusu uchaguzi wa mwaka huu kuwa na mapingamizi mengi na rufaa nyingi ambazo zilipelekea wengi kuenguliwa lakini tume hiyo hiyo iliwarudisha wagombea karibu wote wa Chadema na vyama vingine iweje leo maada ya matokeo wasema sio huru na viongozi wengi walipongeza sana kitendo hicho.
Ngelela alihoji tume waliyopongeza baada ya kurejeshwa ni tofauti na iliyotangaza matokeo ya uchaguzi mkuu je Uhuru ule na huu ni tofauti baada ya matokeo ya uchaguzi?
Aliwakumbusha Chadema kazi ya kutafuta ushindi haitaji maneno mengi CCM ilitafuta ushindi kwa kipindi Cha miaka yote wakati chadema wanajimbo mkoani hapa hatukuiachia tume kutafuta ushindi kwani kazi yake ni kuratibu na kusimamia uchaguzi na kutangaza mshindi na zoezi la kutafuta mshindi ni kazi ya chama Cha siasa.
Alisema kuwa chadema wasifikiri tume uchaguzi kazi yake ni kuwatafutia ushindi vyama vya siasa waache malalamiko ambayo hayana maana kipindi hiki.