Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wagombea Urais kutoka vyama 10 alipokuwa akiwasili kwa katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijni Dodoma kwa ajili ya kukabidhiwa Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akipokea Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akionesha Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.
Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akipokea Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Umakamu wa Rais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Kiti cha Umakamu wa Rais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akionesha Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Umakamu wa Rais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya kutangazwa mshindi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.
Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli akizungumza na Wageni mbalimbali waliofika katika hafla fupi ya kukabidhiwa Cheti cha Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.
Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza Makamu wa Rais Samia Suluhu mara baada ya kukabidhiwa Cheti cha Ushindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage,akizungumza wakati wa kumkabidhi Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais Rais Mteule Dkt.John Magufuli baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Wilson Mahera,akitoa taarifa kuhusu uchaguzi uliofanyika wakati wa kumkabidhi Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais Rais Mteule Dkt.John Magufuli baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Mwakilishi wa watazamaji wa Uchaguzi wa Kimataifa Rais mstaafu wa Burundi Silvester Ntibantunganya akielezea jinsi uchaguzi ulivyokuwa huru na haki kwa kufuata Demokrasia wakati kukabidhiwa Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais Rais Mteule Dkt.John Magufuli baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Mgombea Urais kutoka Chama cha ADC Queen Sendiga,akitoa pongezi kwa Rais Mteule huku akiahidi kushirikiana naye katika kuijenga Tanzania wakati wa kukabidhiwa Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais Rais Mteule Dkt.John Magufuli baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Baadhi ya Makatibu wakuu kutoka katika Wizara mbalimbali wakifatilia hafla ya Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakati akipokea Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Wanachama wa CCM na Viongozi wa Chama hicho waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa kwa Cheti cha Ushindi kwa baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Kikundi cha ngoma kutoka Hombolo kikitoa burudani wakati wa kukabidhiwa Cheti cha ushindi kwa Rais Mteule Dkt.John Magufuli hafla iliyofanyika leo katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi (NEC) iliyopo Njedengwa jijini Dodoma
………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
TUME ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imemkabidhi vyeti vya Mshindi wa kiti cha Rais kwa Mteule Dkt.John Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.
Akitoa neno fupi jijini Dodoma kwenye Ofisi za NEC Njedengwa mara baada ya kukabidhiwa cheti hicho,Rais Mteule Dkt.John Magufuli,amewashukuru watanzania wote kwa kumuamini na kumchagua kwa kura nyingi za kishindo kuwa Rais kwa miaka mitano tena hivyo nitafanya kazi usiku na Mchana ili nitimize mahitaji ya watanzania wote
“Napenda kuwashukuru watanzania wote kunipatia kura nyingi na kukipa ushindi Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa wabunge na madiwani,hivyo nina deni kubwa kwa watanzania wote waliotuamini kupata asilimia 84.4 ni Imani kubwa ,Imani hiyo nitatumia kwa kufanya kazi usiku na mchana.” amesema Dkt.Magufuli.
Aidha Dkt.Magufuli amesema kuwa ana deni kubwa kwa watanzania wote walimuchagua na ambao hawakumchagua hivyo anamuomba Mungu amsaidie pamoja na viongozi wake katika Muhula huu ili aweze kutimiza malengo yake kwa wananchi.
” Niseme kuwa ushindi huu sio wangu wala wa CCM bali ni wa watanzania wote walionipigia kura na ambao hawajanipigia kura wote nawaahidi kuwatimizia mahitaji yote bila kujali Chama,Itikadi za Dini,rangi wala kabila”ameongeza Dkt.Magufuli.
Dkt.Magufuli ameipongeza NEC kwa kazi kubwa walioyoifanya ikiwemo ya kutangaza matokeo kwa haraka hali iliyochangia kuondoa sintofahamu kwa wananchi .
Dk.Magufuli amewashukuru wagombea wa vyama vya upinzani walioshiriki katika kinyanganyiro cha kugombea urais huku akiahidi kushirikiana nao .
“Siasa siyo vita wala siyo ugomvi na katika hilo napenda kuwaahidi kuwa nitashirikiana nanyi kwani maendeleo hayana chama,nitaheshimu na kuzingatia maoni yenye kuleta maendeleo nchini.”amesema Dkt.Magufuli
Awali Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema kuwa,Dkt.Magufuli na mama Samia wamekabidhiwa vyeti hivyo kutokana na Ushindi walioupata katika uchaguzi Mkuu.
“Ili kuweza kuhitimisha zoezi la uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa nafasi ya Rais na kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya 68 ya kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge za mwaka 2020 na leo Novemba Mosi Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawakabidhi wateule wa CCM vyeti vya Ushindi wao.” amesema Jaji Mstaafu Kaijage
Akitoa taarifa ya hali ya Uchaguzi Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Wilson Mahera amesema kuwa uchaguzi umefanyika katika majimbo 264 ambapo majimbo 50 ni Zanzibar na 214 tanzania bara.
Aidha amesema kuwa katika majimbo hayo kata 4 hazikufanya uchaguzi kutokana na wagombea watatu kufariki kabla ya uchaguzi huku katika kata moja kukiwa na changamoto iliyokuwa nje ya uwezo wao kwa wakati huo.
Dkt.Mahera amesema kuwa Tanzania inatumia mfumo ambao mgombea anayepata kura nyingi ndio anayeteuliwa na kuwa chama ambacho kimepata angalau asilimia 5 ya wagombea wake ndio watakaopewa viti maalum.
Naye Mwakilishi wa watazamaji wa Uchaguzi wa Kimataifa Rais mstaafu wa Burundi Silvester Ntibantunganya amesema kuwa uchaguzi wa Tanzania ulikuwa huru na uliofuata demokrasia.
“Dunia imeshuhudia uchaguzi Wenye demokrasia ya hali ya juu na ni matumaini yangu kuwa wengi tumejifunza na kujionea neema iliyopo ya amani na utulivu,”amesema
Kwa upande wa Mgombea Urais wa Chama cha ADC Queen Sendiga amesema kuwa wanampongeza Rais Mteule Dkt.Magufuli kwa kupata ushindi wa kishindo na amemshukuru kwa kuendesha uchaguzi mkuu kwa njia ya demokrasia na amani.
Sendiga amesema kuwa kura zake hazikutosha hiyo sio sababu ya yeye kushindwa kishirikiana na Serikali katika kuijenga Tanzania na kuahidi kuendelea kusimama naye katika kuwatumikia watanzania.
“Utofauti wa vyama si uadui,nakubaliana kuanza upya kushirikiana kwa vitendo na Viongozi waliopo madarakani Katika kuanza kwa matumaini mapya ya miaka mingine mitano ijayo,”amesema Sendiga
Aidha Sendiga amemuomba Rais Mteule Dkt.Magufuli kuwasaidia kuwapa ruzuku ya fedha kwa vyama vyote vya siasa nchini ili viweze kujiendesha.