Watu wote ulimwenguni wanahitaji maendeleo. Hivyo wanapomuona mtu fulani anawaletea maendeleo humpenda, humuamini na kumchagua awe kiongozi.
Kwenye uchaguzi wa 2015, Rais Dkt. John Pombe Magufuli alijipatia kura 8,882,935 ikiwa ni aslimia 58.46 huku mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa wa chama cha Chadema akijipatia kura 6,072,848 ikiwa ni asilimia 39.97 ya kura zote.
Fahamu kwamba wakati Rais Dkt. Magufuli akipata kura hizo mwaka 2015, alikua akiaminika kwa uchapakazi katika wizara chache alizowahi kuziongoza japokua alikua chini ya Rais mwingine, jambo ambalo huenda lilikua likimkwamisha katika kufanya baadhi ya maamuzi.
Lakini baada ya kupata Urais, kazi alizozifanya katika miaka mitano iliyopita, zimewafanya watanzania kuwa na imani nae zaidi tofauti na hapo awali.
Hivyo basi, ushindi wa kura milioni 12.5 alizozipata sio jambo la kumshangaza mwenye akili kwasababu ndani ya miaka mitano yake ya kazi ameweza kuongeza takriban kura milioni 4 tu, ukilinganisha na zile kura milioni 8 alizozipata mwaka 2015.
Aidha, kitendo cha wapinzani kubadilika kutoka watu wa kupinga uzembe wa serikali na kuwa wapinga mandeleo, ni jambo jingine lililomfanya Rais Magufuli aweze kukubaliwa na wapiga kura milioni 4 zaidi.
Kwa mtazamo wangu, Rais Dkt. Magufuli angeweza kupata kura nyingi zaidi endapo wapiga kura wote wangejitokeza kuchagua viongozi Oktoba 28, 2020.