Mnamo Januari 2020 Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliitangazia dunia kwamba mwaka huu atahakikisha Tanzania inafanya uchaguzi huru na wa haki.
Ili kutimiza azma yake, Rais Dkt. Magufuli akaitaka hazina iipe Tume ya Uchaguzi wa Taifa (NEC) fedha za kutosha mapema iwezekanavyo ili isiwe tegemezi pindi muda wa uchaguzi utakapowadia.
Pamoja na hilo, Rais Dkt. Magufuli alikataa kabisa kwamba uchaguzi huu usiendeshwe kwa fedha za kusaidiwa kwasababu jambo hilo huenda likapunguza uhuru wa NEC.
Baada ya uchaguzi kumalizika kwa salama na amani, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imetoa ripoti inayosema kwamba uchaguzi huo ulifanyika kwa amani, uhuru na haki.
Aidha, ripoti ya EAC inasema kwamba Timu ya jumuiya hiyo yenye waangalizi wabobezi 59 iliingia nchini tangu Oktoba 21, 2020 na kusambaa kwenye mikoa 13 nchini.
Timu hiyo imevitembelea viti 160 vya kupigia kura kubaini kwamba uchaguzi umekidhi viwango vyote vya kimataifa.
Hatuna la kufanya isipokua kukupongeza Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahadi yako adhimu.
Hakika umeonesha kwamba wewe ndio mlinzi wa demokrasia ya Taifa letu.