…………………………………………………………………………..
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEKUWA LIKIFUATILIA KWA KARIBU
MCHAKATO WOTE WA UCHAGUZI MKUU 2020, KABLA WAKATI NA BAADA YA KUPIGA
KURA. USALAMA ULIIMARISHWA KWA KIWANGO CHA JUU KWA VIPINDI VYOTE HIVYO.
KWA UJUMLA HAKUNA MATUKIO MAKUB WA YA AJABU YALIYOTOKEA YA KUWEZA
KUATHIRI MCHAKATO MZIMA WA UCHAGUZI MKUU.
JESHI LA POLISI LINAWAPONGEZA WADAU WOTE WA UCHAGUZI AMBAO WALIKUWA
WAKITOA TAARIFA MBALIMBALI ZA WATU WALIOKUWA WAKIJARIBU KUPANGA
NJAMA ZA FUJO AU KUPANGA KUFANYA VURUGU AMBAO WALIKAMATWA NA
KUHOJIWA NA BAADAE KUACHIWA KWA DHAMANA WAKATI UPELELEZI UKIENDELEA .
HATA HIVYO BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZI KUTANGAZWA JESHI LINAENDELEA
KUFUATILIA MIENENDO NA TAARIFA ZA WATU MBALIMBALI AMBAO INADAIWA BADO
WANA MIPANGO YA KUTAKA KUFANYA FUJO AU KUFANYA VITENDO VYA KIHALIFU.
JESHI LINATOA ONYO KALI NA HALITAMVUMILIA MTU YEYOTE AU KIKUNDI CHA WATU
KITAKACHOBAINIKA KUANDAA MIPANGO AU NJAMA ZA KUFANYA VITENDO
VYOVYOTE AMBAVYO NI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI. JESHI LINAENDELEA KUTOA
WITO KWA WANANCHI WEMA KUENDELEA KUTOA TAARIFA MBALIMBALI ZA
WAHALIFU ILI WAKAMATWE MAPEMA KABLA HAWAJATENDA UHALIFU, JESHI
LINASHAURI WANANCHI WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO ZA KAWAIDA NA ULINZI
UMEIMARISHWA.
IMETOLEWA NA;
Muliro JUMANNE MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA