Na.Alex Sonna,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Dkt.John Pombe Magufuli kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi mno wa kura 12,516,252, akifuatiwa na Tundu Lisu wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA) mwenye kura 1,933,271 huku Bernard Membe kutoka Chama cha ACT-Wazalendo akiwa amepata kura 81,129
Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema kuwa jumla ya waliojiandikisha ni 29,754,669, na kura halali zilizopigwa ni 14,830,195 huku kura 261,755 zikikataliwa.
”Tume inamtangaza Dkt.Magufuli kuwa Rais wa Tanzania amepata kura nyingi halali kuliko wagombea wengine wote na tunamtangaza Mama Samia Hassan Suluhu kuwa Makamu wa Rais wa Tanzana”amesema Jaji Mstaafu Kaijage
Jaji Mstaafu Kaijage amesema kuwa Rais Mteule pamoja na makamu wake watakabidhiwa cheti cha ushindi siku ya Jumapili