Timu ya Iringa all star veteran (IASV) ya mjini Iringa ikiwa imetoka katika mechi ya kila ya kujiandaa kwa ajili ya bonanza litakalofanyika jijini Dodom likaloshirikisha timu 24 kutoka mikoa 8 ya Tanzania Bara.
******************************************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Timu ya Iringa all star veteran (IASV) ya mjini Iringa imejipanga vyema kuibuka kifedha katika bonanza litakalofanyika jijini Dodom likaloshirikisha timu 24 kutoka mikoa 8 ya Tanzania Bara.
Akizungumza katika mazoezi ya mwisho yaliyofanyika katika viwanja vya chuo cha Mkwawa nahodha wa timu hiyo Lissa Mwalupindu alisema kuwa wachezaji wote wa timu hiyo wamefanya mazoezi na wapo timamu kuhakikisha wanaibuka mabingwa kwenye bonanza hilo
Alisema kuwa timu hiyo inawachezaji wengi wazoefu na wanauwezo mkubwa wa kucheza mpira na kupata ushindi kwenye bonanza hilo.
“Timu hii inawachezaji wengi waliocheza ligi kuu, ligi daraja la kwanza, la pili na ngazi ya mkoa ambao wamefanya mazoezi kwa muda mrefu na wamekubaliana kurudi na kombe hilo Mkoani Iringa, ili kutoa hamasa ya kwa vijana kuwa na hari ya ushindani kupitia wao kama kioo”
Alisema kuwa bonanza hilo litakaloshirikisha timu kutoka mikoa nane ambayo ni Pwani, Iringa, Dar es Salaam, Morogoro, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na wenyeji Dodoma.
Nao wachezaji wa timu hiyo Davis Wapalila na Abissay Stesheni Jr walitoa onyo kwa timu binzani kujipanga kwa kuwa timu hiyo ipo timu na inaenda kuchukua kombe na sio kushiriki bonanza hilo.
“Sisi wachezaji tupo sawa kwelikweli na tumejipanga kuhakikisha tunaibuka kuwa mabingwa wa bonanza hilo ambalo kwa mara ya kwanza limezikutanisha timu nyingi kutoka mikoa nane ya Tanzania Bara”walisema
Naye msemaji wa timu hiyo ya Iringa all star veterani Denis Mlowe alitoa tahadhari kwa timu pinzani wajipange kwelikweli kwa kuwa timu ya Iringa all stars veterani wanatimu ya ushindani na wamefanya mazoezi muda mrefu na wamejipanga kushinda kombe hilo la bonanza hilo.
“Hawa wazee wako vyema kuhakikisha wanatoa dozi kwa timu yoyote hivyo lengo ni kushinda bonanza hilo ambalo tumelichukulia umuhimu mkubwa na kuwafundisha vijana jinsi ambavyo tulikuwa tunacheza zamani” Alisema
Kwa upande wake Mratibu wa timu hiyo ya Iringa all stars veterani Adv.Lupyana Massawa alisema kuwa wachezaji wote wa timu hiyo watakuwepo kwenye bonanza hilo isipokuwa wachezaji watatu waliopata majeruhi ambao ni Humphrey Ndale, Yohana Tembe na Petro Mrope lakini wachezaji wengine wote wapo vizuri kabisa kwa ajili ya bonanza hilo
Aidha Massawa Aliongeza kuwa wachezaji watakaosafiri na timu ni:
- Attanas Maginga, 2. Adv. Evalisto Myovela, 3. Lissa Mwalupindi, 4. Tumaini Abbisai Stephen, 5. Pendo Mapunda, 6. Abuu Silia, 7. Ally Ngalla, 8. Steve Lihawa, 9. Omary Daudi, 10. Hasan Ussi, 11. Rashid Msigwa, 12. Ally Msigwa, 13. Dikson Kiboye, 14. Denis Mlowe, 15.Khalid Fungabrek, 16.Pendo Mapunda, 17. Nicholaus Shari, 18.Petro Mrope, 19.Fredy Mgunda, 20.Davis Wapalila, 21.Ramadhani Shemhilu,22. Godlisten Mlaki,23.Ally Lwambano,24.Lusekelo Kibona, 25.Simba Yusuph