Picha: wapiga kura wakiwa wamejipanga kwenye mstari huku zoezi la upigaji kura likiwa linaendelea kituo cha kupigia kura Mwamasabi, kata ya Lamadi.
………………………………………………………………….
Wananchi Jimbo la Busega wamejitokeza kwa wingi kupiga kura katika vituo mbalimbali vilivyopo jimboni humo. Mapema kuanzia saa moja kamili (1:00) Asubuhi vituo vilikuwa vimefunguliwa tayari kwa wapiga kura kuanza kuchagua viongozi wanaowataka.
Wapiga kura wapatao 124,316 ambao walijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura wataweza kupiga kura. Jumla ya vituo 325 vilivyopo katika kata zote 15 Jimbo la Busega vimefunguliwa na zoezi la kupiga kura linaendelea. Aidha, ulinzi umeimarishwa ili kutoa fursa kwa wananchi kuweza kuchagua viongozi wanaowataka kila kituo cha kupigia kura.