Home Michezo SIMBA YAPOKEA KICHAPO KUTOKA KWA MAAFANDE RUVU SHOOTING

SIMBA YAPOKEA KICHAPO KUTOKA KWA MAAFANDE RUVU SHOOTING

0

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Simba imezidi kufanya vibaya kwenye mechi hivi karibu baada ya kupekea tena kichapo cha bao 1-0 na maafande wa Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Goli la Ruvu Shooting lilifungwa na Nyota wao Zullu Maganga mnamo dakika 36 ya mchezo kipindi cha kwanzo.

Mchezo huo ulikuwa na matukio mbalimbali ndani ya uwanja baada ya mchezaji wa Simba kuchezewa rafu mbaya na mchezaji wa Ruvu Shooting na kuamuliwa penati lakini wachezaji wa Ruvu Shooting hawakupendezwa na maamuzi ya refa hivyo kuanza kutunishiana ubavu na wachezaji wa Simba na kupeleka mchezaji wa Ruvu Shooting kupewa kadi Nyekundu.

Mchezo huo kwa Simba ni wa pili mfululizo kufungwa baada ya wiki iliyopita kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa maafande wa Tanzania Prison